“Acacia Tufanikiwe Pamoja Cycle Challenge 2015.”
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
MBIO ZA BAISKELI KANDA YA ZIWA – 2015.
Kahama. June 13, 2015:
MIKOA YA SHINYANGA NA MWANZA YAENDELEA UBABE MBIO ZA BAISKELI.
Washiriki
wa mbio za baiskeli zijulikanazo kama “Acacia Tufanikiwe Pamoja Lake
Zone Cycle Challenge” kutoka mikoa ya Shinyanga na Mwanza wameendelea
kuudhihirisha umma wa wakazi wa kanda ya ziwa na watanzania kwa ujumla
kuwa mpaka sasa hawana mpinzani baada ya washiriki wa mbio hizo kuibuka
kidedea katika fainali za kumtafuta mshindi wa kanda hiyo.
Washiriki
wa mikoa hii miwili wamejinyakulia nafasi zote za juu na hivyo
kuwashinda wenzao wa mikoa mingine ya Kanda ya ziwa ikiwemo Kagera,
Mara, Geita
na Simiyu.
Katika
mbio za wanaume za umbali wa kilometa 156.6 kutoka Kahama mpaka Tinde
na kisha Kurejea Kahama, mshindi wa mwaka jana Masunga Duba (Mwanza)
aliibuka
tena kidedea huku nafasi ya pili ikichukuliwa na Lupilya
Hamis(Shinyanga) na nafasi ya tatu ikimuendea Kulwa Tuki(Shinyanga),
washindi hawa wamejinyakulia kitita cha pesa taslimu Sh1,500.000/- kwa
mshindi wa kwanza, Sh1,200.000/= mshindi wa pili na Sh800,000/=
kwa mshindi wa tatu.
Kwa
upande wa mbio za wanawake za umbali wa kilometa 80, kutoka Kahama
mpaka Mwakata Kisha kurejea Kahama, timu ya mkoa wa Mwanza imedhihirisha
kuwa
wao bado ni mabingwa kwa kuibuka tena washindi wa mbio hizo, huku
mshindi wa mbio za Mwaka jana Martha Antony, akiibuka mshindi wa kwanza
akifuatiwa na Laulensia Luziba na nafasi ya tatu ikienda kwa Veronica
Simon. Washindi hao wamepata zawadi ya pesa taslimu
Sh1,200.000/= kwa mshindi wa kwanza, Sh800,000/= mshindi wa pili na
Sh600,000/= mshindi wa tatu.
Mbio
hizo ambazo zimeandaliwa na Chama cha Baiskeli Tanzania (CHABATA) kwa
udhamini wa kampuni ya uchimbaji wa Madini ya Acacia, inayomiliki migodi
ya North Mara, Bulyanhulu na Buzwagi, yote ikiwa mikoa ya kanda ya
ziwa, kupitia mpango wake wa Tufanikiwe Pamoja ikiwa ni mara ya pili
sasa ambapo mashindano ya mwaka huu yameonyesha mafanikio makubwa
kutokana na maandalizi mazuri yaliyofanyika.
Akizungumza
na washiriki wa mashindano hayo Mkuu wa wilaya ya Kahama Benson Mpyesa,
ambaye alikua mgeni rasmi wa fainali hizi, amesema ana imani kuwa
mashindano hayo yatasaidia kuibua vipaji ambavyo vitauletea sifa mkoa
wa Shinyanga, Kanda ya ziwa na hata taifa kwa ujumla kwani baiskeli kwa
maeneo hayo ndiyo jadi yao.
Awali
akimkaribisha Mkuu wa wilaya kuzungumza na washiriki hao, Makamu wa
Rais wa Acacia Deo Mwanyika amesema kampuni ya Acacia imekuwa ikifanya
shughuli
za uchimbaji unaojali na ndio maana iliona vyema kuweka udhamini wake
pia katika mchezo wa baiskeli, “toka tuanze huu sasa ni mwaka wa pili na
tunayaona mafanikio makubwa kwani hata maeneo ambapo mchezo huu ulikuwa
hauchezwi sasa unachezwa, hali ambayo imeongeza
hamasa na idadi ya washiriki.”
Aidha
Makamu wa Rais huyo wa Acacia amesema mipango ya kampuni kwa sasa ni
kuona pia inashiriki katika kuendeleza michezo mingine ikiwemo na soka.
Mwisho.
Mmoja wa washiriki wa mbio hizo akinywa maji wakati wa mashindano hayo.
Mshindi
wa mbio za Acacia Tufanikiwe Pamoja Lake Zone Cycle Challenge, Masunga
Duba aliyeinua mikono akishangilia mara baada ya kumaliza mbio hizo
akiwa mbele ya wenzake. Mshindi huyo anatoka
mkoa wa Shinyanga.
Makamu
wa rais wa Kampuni ya Uchimbaji wa dhahabu ya Acacia, Deo Mwanyika (wa
kwanza kushoto) akifurahia jambo na Afisa Mkuu wa Uendeshaji wa kampuni
ya Acacia, Mishel Ash, (wa pili kutoka kushoto)
ambaye pia ni kaimu Meneja Mkuu wa Mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu.
Washindi
wa mbio za wanawake (kilometa 80). Aliyesimama katikati ni Martha
antony ambaye ndio aliibuka mshindi wa kwanza, akifuatiwa na Laulensia
Luzuba, (mwenye mtoto) aliyekuwa mshindi wa pili
na Veronica Saimon (wa kwanza kushoto) aliyejinyakulia nafasi ya Tatu.
Washiriki wa mbio za Acacia tufanikiwe pamoja lake zone cycle challenge wakimenyana vikali wakati wa mashindano hayo.
Afisa
mkuu wa uendeshaji wa kampuni ya Acacia Mishel Ash akimvisha medali
mshindi wa mbio hizo Martha Antony wakati wa Hafla ya Kutoa zawadi kwa
washindi.
Mshindi wa pili wa mbio hizo kwa upande wa wanawake
Laulensia Luziba akifurahia zawadi zake na mtoto wake mara baada ya
kukabidhiwa na afisa mkuu wa uendeshaji wa Acacia Mishel Ash.
Meneja mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Philbert Rweyemamu akitoa zawadi kwa washindi wengine wa mbio hizo kwa upande
wa wanawake.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya akimkabidhi zawadi Mshindi wa kwanza wa mbio hizo kwa upande wa wanaume,
Masunga Duba kutoka shinyanga.
Mshindi wa pili wa mbio hizo Ndimi Hamis akipokea zawadi yake kutoka kwa mgeni rasmi.
Washindi wa kwanza wa mbio hizo kwa upande wa wanaume na wanawake wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya
kukabidhiwa zawadi zao.
Mmoja wa wafanyakazi wa Acacia aliyeshiriki mbio maalumu kwa wafanyakazi wa Acacia, akifurahia mara baada ya
kufanikiwa kumaliza mbio hizo.
Makamu wa rais wa Acacia, Deo Mwanyika akifanya mazoezi mepesi muda mfupi kabla ya kuanza kwa mashindano hayo.
Afisa mkuu wa uendeshaji wa Acacia Mishel Ash akiwa tayari kwa mbio hizo.
Washiriki wa mbio za wafanyakazi wa Acacia wakiwa tayari kuanza mbio hizo ambazo zilikuwa zimepewa jina la “Fun race”
|
People (2)
Show details
|
WAKULIMA WASHAURIWA KUWA NA UTARATIBU WA KUKATA BIMA KUEPUKA HASARA
INAYOTOKANA NA MAJANGA
-
Na Said Mwishehe,Michuzi TV
MKURUGENZI Mtendaji Mkuu wa Kampuni inayojihusisha na masuala ya Bima
NewTan Insurance, Nelson Rwihula amesema wakulima...
42 minutes ago
No comments:
Post a Comment