Na Swahilivilla Blog, Washington DC
Tanzanian Muslim Community Washington DC na vitongoji vyake nchini Marekani (TAMCO) imesisitiza umuhimu wa umoja na mshikamao wa kijamii miongoni mwa wanajumuiya hiyo na Watanzania kwa ujumla wanaoishi katika maeneo hayo.
Mwenyekiti wa Tanzanian Muslim Community Ndugu Ali Muhammed Shafi (Picha zote na Abou Shatry)
Hayo yameeelezwa na Mwenyekiti wa TAMCO Ndugu Ali Muhammed Shafi alipokuwa akizungumza na Swahilivilla pembezoni mwa "Siku Ya Familia" iliyoandaliwa na Jumuiya hiyo, Siku ya Jumamosi June 6, jijini Washington DC.
"Lengo kubwa la siku hii ni kuwakusanya pamoja wanachama wa jumuiya yetu na Watanzania wengine wanaoishi katika eneo hili hata kama si wanachama wa jumuiya yetu, kwa lengo la kusisitiza umuhimu wa Familia na mshikamano wa kijamii", alisema Ndugu Shafi, na kuongeza kuwa ni nafasi nzuri ya kujuana khususan kwa watoto.
Aliendelea kusema kuwa mkusanyiko huu ambao hufanyika mara moja kila mwaka una lengo pia la kufanya matayarisho ya mwezi Mrukufu wa Ramadhan, ambapo wanajumuiya huchangisha fedha kwa jili ya futari ya pamoja kwa mwezi mzima wa Ramadhani.
"Tayari TAMCO imeshaandaa kumbi maalum kwa ajili ya futari ya pamoja kwa muda wa mwezi mzima wa Ramadhani na matayarisho yote yameshakamilika, tunachosubiri ni kumkaribisha mgeni huyo Mtukufu" alisema Bwana Shafi, na kuwatolea wito wanajumuiya ambao bado hawajatoa ada zao za uanachama kufanya hivyo, ili kurahisisha na kufanikisha malengo ya jumuiya hiyo.
Akizungumzia malengo ya baadaye ya jumuiya hiyo, Bwana Shafi alisema kuwa wana lengo la kufungua madras kwa ajili ya watoto wanaoish Washington na maeneo ya karibu, ili kuhakikisha kuwa watoto wanapata elimu,malezi na mafunzo halisi ya Kiislamu.
Aliwatolea wito wanajumuiya kuitumia fursa ya mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa ajili ya kuongeza Ibada na Imani ndani ya mwezi huo na katika maisha kwa ujumla.
Siku Ya Familia ya TAMCO (TAMCO Family Day), hufanyika kila mwaka ambapo wanajumuiya hiyo na wengineo hukutanika pamoja kwa siku nzima, ambapo pamoja na mambo mengine, hutoa nafasi kwa watoto kucheza, kufurahi kujuana na kujenga urafiki tangu wakiwa wadogo.
Baadhi ya waumini wa Tanzanian Muslim Community wakiwa katika mkusanyiko wa siku ya familia, ilioandaliwa rasmi na jumuiya hiyo, Siku ya Jumapili June 6, waIslamu Washington DC
Nyuma kabisa aliekuwa muasisi wa zamani wa Tanzanian Muslim Community in Washington DC (TAMCO) Bwana Yusuf Kalala akiwa na Shamis Alhatry, kushoto, Kulia ni Mwenyekiti wa ZADIA, pa moja na Mganga katika sharehe ya familia Day Siku ya Jumamosi June 6, waIslamu Washington DC
Baadhi ya waumini wa Tanzanian Muslim Community wakiwa katika mkusanyiko wa siku ya familia, ilioandaliwa rasmi na jumuiya hiyo, Siku ya Jumapili June 6, waIslamu Washington DC
No comments:
Post a Comment