
Mratibu
wa Bima ya Elimu kwa Uwapendao kutoka Taasisi ya Kifedha ya Bayport
Financial Services, Ruth Bura, kushoto akimkabidhi hundi Latifa Juma
yenye thamani ya Tsh 3,000,000, baada ya mzazi wake Juma Said, aliyekuwa
Mchapa Vitabu wa Shule ya Uhuru Mchanganyiko, jijini Dar es Salaam.
Kulia ni mume wa Latifa, anayeitwa Bakari Msumi. Picha zote kwa Hisani
ya Bayport Financial Services.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
TAASISI ya
Kifedha ya Bayport Financial Services, leo jioni imemkabidhi hundi ya Sh Milioni
tatu (3,000,000), mjasiriamali Latifa Juma, ikiwa ni sehemu ya mafao yake baada
ya mzazi wake Said Juma, kuwa mteja wa Bayport kwa kupitia huduma yake ya Bima
ya Elimu kwa Uwapendao iliyoanzishwa mapema mwaka jana.
Makabidhiano
hayo yalifanyika Makao Makuu ya Bayport Financial Services, Morocco, jijini Dar
es Salaam, huku akisindikizwa na mumewe Bakari Msumi. Akizungumza
katika makabidhiano hayo, Mratibu wa Bima ya Elimu kwa Uwapendao ya Bayport
Financial Services, Ruth Bura, alisema kwamba marehemu Said Juma alikuwa mteja
wao, huku akijiunga pia katika huduma ya bima, ambayo leo imemnufaisha mtoto
wake.

Mratibu
wa Bima ya Elimu kwa Uwapendao kutoka Taasisi ya Kifedha ya Bayport
Financial Services, Ruth Bura, kushoto, akiwa kwenye makabidhiano ya hundi
Latifa Juma yenye thamani ya Tsh 3,000,000, baada ya mzazi wake Juma
Said, aliyekuwa Mchapa Vitabu wa Shule ya Uhuru Mchanganyiko, jijini Dar
es Salaam. Kulia ni mume wa Latifa, anayeitwa Bakari Msumi. Picha zote
kwa Hisani ya Bayport Financial Services.
Alisema
mapema mwaka huu mteja wao alifariki Dunia, hivyo baada ya kupata
taarifa hizo tuliamua kufuatilia na kukutana na mtoto wake Ratifa,
ambaye hapana shaka fao hili linaweza kumuendeleza zaidi na zaidi. “Bayport
Financial Services kama kawaida yetu tumekuwa na lengo la kuwakomboa
wateja wetu kwa kuwapatia mikopo mbalimbali kama vile mikopo ya fedha,
mikopo ya bidhaa ikiwamo huduma yetu mpya ya mikopo ya viwanja vya
Vikuruti, wilayani Kibaha, mkoani Pwani, bila kusahau fao la Bima ya
Elimu ambalo lina umuhimu mkubwa.
“Naomba
Watanzania wote waweke utaratibu wa kujiunga na bima hii ambayo malipo
ya kila mwezi kwa fao la Bronze ni Sh 3500 tu, huku mafao yake yakiwa ni
Sh 1,800,000, huku Makato ya bima ya Silver yakiwa ni Sh 7,000 na fao
lake ni Sh 3,700,000 na Gold akilipwa mteja Sh 7,500,000 wakati makato
yake yakiwa ni Sh 12,000 tu kwa mwezi,” alisema Ruth.
Naye
Ratifa aliwashukuru Bayport kwa huduma zao nzuri, huku akisema mafao ya
baba yake yatachangia kwa kiasi kikubwa kuboresha maisha yake na mama
yake, hususan kwa kuendeleza ujenzi wa nyumba yao.
“Ninachotaka
kufanya ni kuendeleza ujenzi wa nyumba yetu ili mimi na mama yangu
tuishi vizuri, baada ya kufiwa na baba yetu, ambaye leo tumepewa kiasi
hicho cha pesa,” alisema.
Naye
mume wa Ratifa, Bakari Msumi, alisema hajawahi kuona taasisi yenye
huduma nzuri kama Bayport Financial Services, hasa baada ya
kuhakikishiwa malipo ya mafao yam zee wao bila usumbufu wowote, jambo
ambalo ni nadra kwa taasisi nyingi nchini.
“Awali
hatujafahamu kama tunaweza kupata bila usumbufu, ajabu ni kuona sisi
tunapigiwa simu hatua kwa hatua, kuelekezwa njia za kupita, hususan
baada ya kuitwa katika makabidhiano ya hundi,” alisema Msumi na
kuwapongeza Bayport, huku akiwataka Watanzania wote kuchangamkia huduma
zote zinazotolewa na Bayport.
Aidha,
utaratibu wa malipo ya huduma hiyo ya Bima ya Elimu kwa Uwapendao
umepangwa kulipwa kila mwaka, ili kuhakikisha kuwa mafao hayo
yananufaisha walengwa, hususan kwa wale wanaoendelea na masomo katika
shule na vyuo mbalimbali nchini.
No comments:
Post a Comment