Uhakiki
wa vikundi vya vijana vilivyopewa msaada wa mashine na NHC ili
kujiajiri na kusaidia wananchi kupata matofali ya kujengea nyumba bora
umeanza katika Mikoa mbalimbali ukianzia na Mkoa wa Lindi na Mtwara.
Katika hali isiyotarajiwa Mkoa wa Mtwara ambao kwa muda mrefu umekuwa
ukililia kuletewa maendeleo umeshindwa kutumia fursa ya msaada wa
mashine kwa vijana waliyopewa na NHC hali iliyolifanya Shirika kutwaa
baadhi ya mashine ili zipewe vikundi vingine vinavyofanya vizuri
Fuatilia kupitia habari picha hizi ili ufahamu kilichojiri katika mikoa
hiyo ya kusini mwa Tanzania. Leo uhakiki huo unaendelea Mkoani Ruvuma.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Bw. Nicholous Kombe
akimsikiliza Meneja wa Huduma kwa Jamii wa NHC Bw. Muungano Saguya
akimshukuru kwa Halmashauri hiyo kusaidia kikundi cha vijana kwa
kuwawezesha fedha na udongo kwa ajili ya kutengeneza matofaliya
kufungamana. Katikati ni Meneja wa NHC Mkoa wa Lindi Bw. Mussa Patrick
Kamendu.
Jengo
la Ofisi ya kikundi cha vijana cha Narunye(hakuna kutegeana) katika
Halmashauri ya Wilaya ya Lindi Vijijini likiwa limeonwa na Kiongozi wa
mbio za mwenge wa Uhuru kama inavyoonekana. Kikundi hiki kimeshaanza
kupata maombi mengi ya matofali kutoka kwa wananchi wanaohitaji.
Kikundi
cha vijana cha Ruangwa Materials Group katika Halmashauri ya Wilaya
Ruangwa kimeshatengeneza matrofali kwa kutumia mashine ya msaada kutoka
NHC. Halmashauri ya Wilaya hiyo imeamua kuyatumia matofali ya vijana
hawa kujengea zahanati na majengo mengine yanayohitajika katika
Halmashauri zikiwemo nyumba za Waalimu.
Meneja
wa NHC Mkoa wa Lindi Bw. Mussa Patrick Kamendu akitoa mawaidha kwa
kikundi cha vijana cha Narunye kilichopo katika Wilaya ya Lindi vijijini
baada ya kutembelea kikundi hicho kukagua kazi zake.Vijana hawa
wanajihusisha pia na utunzaji mazingira.
Baada
ya Wakurugezi wa Halmashauri za Kilwa na Lindi Vijijini kutokuwa karibu
na vikundi vya vijana, Meneja wa Huduma kwa Jamii wa NHC na Meneja wa
Mkoa wa Lindi waliweza kufanya mazungumzo nao ya kina na hatimaye
wamekubali kuwasaidia vijana waliopewa msaada wa mashine na NHC katika
Halmashauri zao ili waweze kujiajiri. Kulia ni Bi. Oliver Vavunge ambaye
ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Lindi Vijijini na wa
pili kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Kilwa Bi. Maimuna
Mtanda.
Kaimu
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi Bw. Daniel Kaluse hakuwa
nyuma kutembelea kikundi cha Vijana na Maendeleo kilichopo eneo la
Mitwero nje kidogo ya Manispaa hiyo ili kuwapa moyo na kufahamu
maendeleo yao akiwa ameandamana na ujumbe wa NHC.
Meneja
wa NHC Mkoa wa Mtwara Bw. Joseph John akitoa taarifa ya Mkoa kwa Meneja
wa Huduma kwa Jamii wa NHC ya maendeleo ya vikundi vya vijana
waliosaidiwa mashine na NHC . Katika taarifa yake Meneja huyo
alisikitishwa na vijana wa Mkoa wa Mtwara kushindwa kutumia kikamilifu
msaada huo na akalaumu Halmashauri za Mkoa huo kushindwa kushiriki
kikamilifu katika programu hiyo ya kusaidia vijana.
Meneja
wa Huduma kwa Jamii wa NHC Bw. Muungano Saguya akikemea na hatimaye
kukinyanganya mashine kikundi cha Likonde katika Manispaa ya Mtwara kwa
kuifungia stoo mashine waliyopewa msaada na NHC bila kufanya kazi
iliyokusudiwa ya kufyatua matofali. Mashine hiyo itapewa kikundi kingine
ili itumike kikamilifu.
Meneja
wa Huduma kwa Jamii wa NHC Bw. Muungano Saguya akiwa Wilayani
Tandahimba akikagua matofali yaliyotengenezwa na kikundi cha vijana cha
Maendeleo Group kilichopewa msaada wa mashine na NHC. Kikundi hiki
kinasubiri kulipwa na Halmashauri matofali hayo yanayotarajiwa kujengea
nyumba za waalimu.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Tandahimba Bw Dennis Mwaitete akielezea
mkakati wa Halmashauri yake wa kusaidia vijana ulivyo alipotembelewa na
ujumbe wa NHC uliokuwa ukihakiki vikundi vya vijana Mkoani Mtwara.
Kikundi
cha vijana cha Umoja Lekanelo kilichopo Wilaya ya Newala kilichoshindwa
kutumia kikamilifu mashine ya msaada kilichopewa na NHC kiliweza
kupokonywa mashine hiyo jana. Wilaya ya Newala ina shughuli za madini na
kilimo cha korosho kiasi cha kuwafanya vijana kushindwa kujihusisha
kikamilifu na mradi wa kufyatua matofali.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala Bw. Marx Kamaoni
akizungumza na ujumbe wa NHC uliofika Ofisini kwake kuhamasisha
Halmashauri za Wilaya kusaidia vikundi vya vijana vilivyopewa msaada wa
mashine za kufyatulia matofali na NHC.
Vyombo
vya habari vimehusishwa katika uhakiki huu na hapa Mkurugenzi Mtendaji
wa Halmashauri ya Newala Bw. Marx Kamaoni akiongea na waandishi wa
habari kuelezea mkakati wa Halmashauri yake kusaidia vijana.
Kikundi
cha Vijana cha For Energy Group kilichopo Wilayani Masasi kilitembelewa
na baada ya kuridhishwa na utendaji wake NHC ilikiongezea mashine mbili
zilizopokonywa vikundi vingine vilivyoshindwa kuzitumia Wilayani Newala
na Masasi Vijijini. Hii ni nyumba iliyojengwa na kikundi hicho Wilayani
Masasi.
Meneja
wa Huduma kwa Jamii wa NHC Bw. Muungano Saguya akivionya vikundi vya
vijana vya Nayoden na Mangaka Wilayani Nanyumbu waliokula fedha ya mtaji
waliopewa na NHC ambapo aliamuru kuchukuliwa kwa mashine zao na kuwapa
muda wa kujiandaa. Aliwataka kuziomba mashine hizo kwa maandishi
watakapokuwa tayari kuzitumia. Mashine hizo zilifungiwa Ofisi ya Kata ya
Mangaka kwa muda wa miezi nane wakisubiri kupata fedha nyingine kutoka
NHC.
Mashine
iliyopokonywa vijana wazembe Wilayani Nanyumbu ikipandishwa katika gari
baada ya vijana hao kuzembea kuitumia na kuifungia Ofisi kwa muda
mrefu.
No comments:
Post a Comment