Rais
wa TFF Jamal Malinzi akizungumza na waandishi wa habari wakati
akimtangaza kocha mpya wa Stars, Charles Boniface Mkwasa. (Picha na
Francis Dande)
Aliyekuwa kocha wa timu ya taifa 'Taifa Stars', Mart Nooij akizungumza na waandishi wa habari baada ya kibarua chake kuota mbawa.
Rais wa TFF akitangaza kocha mpya wa taifa stars, Charles Boniface Mkwasa.
Aliyekuwa kocha wa timu ya taifa 'Taifa Stars', Mart Nooij akitafakari jambo wakati malinzi akitangaza nafasi yake kuchukuliwa na kocha Charles Boniface Mkwasa.
Aliyekuwa
kocha wa timu ya taifa 'Taifa Stars', Mart Nooij akiangalia saa yake
muda mfupi baada ya kutupiwa virago na TFF na nafasi yake kuchukuliwa na
kocha mzawa Charles Boniface Mkwasa.
..........................................
Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania - TFF, Jamal Malinzi leo
ameagana rasmi na aliyekua kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania
(Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager,
mholanzi Mart Nooij.
Akiongea
na waandishi wa habari leo katika hoteli ya Tansoma, Malinzi amesema
wameamua kuagana nae mbele ya vyombo ya habari kama iliyofanyika pia
wakati wa utambulisho wake wakati wa kuanza kazi.
“Mpira
wa miguu unachangamoto nyingi, watanzania tunasafari ndefu katika
mafanikio ndio maana TFF imeanza kuwekeza katika soka la vijana, sababu
ndio msingi wa kuwa na timu bora ya Taifa” alisema Malinzi.
Duniani
kote chimbuko la timu bora ni soka la vijana na watoto, tukiwa na
vijana wengi walioanza kucheza mpira katika umri mdogo wanapofikia umri
wa kuchezea timu ya Taifa tutakua na kikosi bora.
Nchi
za wenzetu inapofikia kocha kuita wachezaji wa timu ya Taifa anakuwa na
wigo mpana, kwetu sisi wachezaji wanocheza soka nje ya nchi
wanahesabika, hivyo ni lazima tuanze kuwekeza kwenye soka la vijana
TFF ilishaanza mkakati huo ndio maana kuna timu za U13, U15 ambazo
zitakua zikiingia kambini na kucheza michezo ya kirafiki ndani ya nje
kwa lengo la kupata uzoefu kabla ya kushiriki kuwania kufuzu kwa fainali
za vijana mwaka 2016.
Kikosi cha U15 kinatarajiwa kufanya ziara mwezi Disemba mwaka huu katika
nchi za Malawi, Zambia, Zimbambwe, Botswana na Afrika Kusini, kisha
mwakani mwezi April 2016 kitaenda Rwanda, Burundi, Uganda na Kenya
kucheza michezo ya kirafiki.
Naye Mart Nooij aliyekua kocha wa Taifa Stars, akiongea na waaandishi wa
habari alisema anawashukuru watanzania wote, serikali, wadau wa mpira
wa miguu nchini na TFF kwa sapoti waliyompatia wakati akiwa kocha mkuu
wa timu ya Taifa.
Nooij alisema alifurahia maisha yake akiwa Tanzania kwa kipindi chote
alichokua akifundisha timu ya Taifa, lakini kwa sababu imefikia mwisho
wa ajira yake hana jinsi anaondoka, lakini ataendelea kuikumbuka
Tanzania na watanzania wote kila siku kwa ukarimu wao.
Wakati huo huo Rais wa TFF. Jamal Malinzi amemtangaza Charles Mkwasa
kuwa kocha mpya wa Taifa Stars akisaidiwa na kocha Hemed Morocco,
Mkwasa ambaye ni kocha wa Yanga na Morocco kocha wa Mafunzo watafanya
kazi kwa kipindi cha miezi mitatu ambayo timu ya taifa itakua na michezo
ya kuwania kufuzu kwa CHAN na AFCON.
Kocha Mkuu mpya wa timu ya taifa ‘Taifa Stars’ Charles Boniface
Mkwasa (wa pili kushoto) akitoka katika mazoezi ya timu yake ya Yanga kwenye Uwanja
wa Karume jijini Dar es Salaam leo. Mkwasa ametangazwa leo kuwa kocha mkuu wa
Stars kushika mikoba ya Mdachi Mart
Nooij aliyetimuliwa. (Picha na Francis Dande)
Malinzi amesema uteuzi wa makocha hao wazawa umezingatia vigezo vya
makocha wa timu ya Taifa kuwa na leseni A ya ukocha kutoka CAF au
zinazofanana kutoka mashiriksho mengine duniani wanaozifanyia kazi,
jambo ambalo makocha hao wazawa wamekizi.
Kocha Mkwasa atakua akipewa hudumu zote na masilahi (zikiwemo posho)
alizokuwa anapewa kocha aliyeondoka, pia amepewa nafasi ya kuchagua
benchi lake la ufundi la kufanya nalo kazi, hivyo nawaomba wadau wa
mpira wa miguu na watanzania kwa ujumla tuwape sapoti makocha hao
wazawa” aliongeza Malinzi”
Aidha Kamati ya utendaji ya TFF Iimemteua Alhaj Ahmed Mgoyi kuwa mratibu
wa timu ya Taifa, lengo la uteuzi huo wa Mgoyi ni kuwa kiunganishi kati
ya kamati ya Utendaji na timu ya Taifa.
U15 YAINGIA KAMBINI
Timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 15 ya Tanzania,
imeingia kambini jana na kuanza mazoezi leo katika uwanja wa Karume
kujiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya kombaini U15 ya mkoa wa Mbeya
siku ya jumapili.
Kikosi hicho kilicho chini ya makocha Bakari Shime na Peter Manyika
kitacheza mchezo huo kwa lengo la waalimu kupatawa fursa ya kuwaona
vijana hao na kuwaongeza wengine watakaoneka katika kikosi hicho.
U15 ni mpango wa TFF kuandaa kikosi kizuri chenye ubora kuelekea kuwania
kufuzu ka fainali za vijana Afrika mwaka 2017 zitakazofanyika nchini
Madagascar, ambapo vijana hao watakua na umri wa miaka 16 kufikia
mwakani wakati michezo ya kuwania kufuzu itakaponza mwezi Julai, 2016.
NB: Kesho siku ya jumatano kocha mpya wa Taifa Stars, Charles Mkwasa na
msaidizi wake Hemed Moroco wataongea na waandishi wa habari saa 5:30
asubuhi katika ukumbi wa mikutano wa TFF uliopo Karume.
Waandishi wote wa habari mnaombwa kuhudhuria bila kukosa.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
No comments:
Post a Comment