KUFUATIA
mafanikio makubwa yaliyopatikana katika Msimu wa Pili wa Coke Studio
Africa, Kampuni ya Coca-Cola kwa kushirikiana na Shirika la Ndege la
Kenya, inayo furaha kutangaza kuanza tena msimu wa tatu wa burudani ya
muziki maarufu kwa jila la Coke Studio Africa. msimu huu utajumuisha
wanamuziki wakali 26 barani Afrika huku nyimbo mpya 52 kutumbuizwa
ikiambatana na maonyesho 9 ya wanamuziki wanaotamba hapa duniani.
Maonyesho
hayo ya muziki ya Coke Studio Africa ni tofauti na mengine ya aina hiyo
yanayolenga zaidi kupatikana mshindi. Badala yake, maonyesho haya
yanalenga kujumuisha pamoja vipaji tofauti vya wanamuziki mbalimbali
kutoka barani Afrika. Aidha, yanatoa fursa kwa wasanii wanaochipukia
kufanya pamoja kazi zao na wanamuziki nguli wa ndani na wale wa ngazi za
kimataifa.
Alikiba |
Msimu huu
unaozinduliwa utawakutanisha wanamuziki kutoka katika nchi za Tanzania,
Msumbiji, Kenya, Uganda na Nigeria, na kwa mara ya kwanza wasanii hawa
wataweza kukonga nyoyo za wapenzi wa muziki kwa kushirikiana katika
staili ya kipekee ijulikanayo kama mash-ups – ambayo inatawala kwa sasa
katika tasnia ya muziki duniani. “Kufurahia muziki wa Kiafrika” ikiwa
ndiyo kiini kikuu cha burudani hiyo, msimu huu mpya wa Coke Studio
Africa utawakutanisha wasanii maarufu ambao wameonyesha mafanikio
makubwa katika kazi zao, na pia maonyesho hayo yatawaleta pamoja wasanii
nyota wanaochipukia katika ulimwengu wa muziki.
Chini
ya ushirikiano huo mpya na Kampuni ya Coca-Cola, Shirika la Ndege la
Kenya kwa upande wake litawasafirisha wasanii wote na waandaaji wa
muziki wanaoshiriki katika Msimu wa Tatu wa Coke Studio Africa. Mpango
huo wa ushirikiano wa makampuni haya makubwa unatokana na imani ya
kwamba hatua hiyo itajenga msingi wa ubia muhimu wa kufanya kazi kwa
pamoja.
Vanessa Mdee |
Akizungumzia
juu ya Coke Studio Africa Msimu wa Tatu, Meneja Bidhaa wa Coca-Cola
Tanzania, Maurice Njowoka alisema: “Lengo letu ni kuufanya na kuwezesha
namna ambayo muziki unavyoweza kuchukua nafasi katika kukonga nyoyo za
watu katika Bara letu. Coke Studio Msimu wa Tatu si kwa ajili ya
kuwakutanisha tu wanamuziki wa Afrika, bali pia maonyesho haya yanatoa
fursa ya pekee ya ushirikiano ambao ni imani yetu kuwa wateja wetu
pamoja na umma kwa ujumla wangependa kuusikia.”
Bwana
Njowoka alisema kwamba, msimu huu wa Coke Studio Africa Msimu wa Tatu
unatarajiwa kuwa na mambo makubwa na mazuri zaidi na utatoa fursa ya
kipekee kwa kila mtu kuburudika zaidi. Miongoni mwa nyota watakaotoa
burudani msimu huu ni pamoja na Ali Kiba, Vanessa Mdee Ben Pol na Fid Q
kutoka Tanzania.
Wengine
ni AVRIL, Wangen, The Unstoppable Elani na Juacali kutoka Kenya il-hali
kwa mara ya kwanza Malkia wa Afrika, 2Face Idibia, ataonyesha vitu
vyake motomoto akiungana na nyota wengine kama vile Yemi Alade. Magwiji
wengine katika tasnia hiyo ya muziki watakaokuwapo ni pamoja na Dr. Jose
Chameleone, Neyma, Dama Do Bling kutoka Msumbiji.
Mkuu
wa Idara ya Masoko wa Shirika la Ndege la Kenya, Jacquie Muhati, alisema
ya kuwa ushirikiano kati ya shirika lake na Kampuni ya Coca-Cola utatoa
fursa kwa wasanii hao wa Afrika kufurahia huduma nzuri za usafiri
zinazotolewa na shirika hilo. “Hii ni fusa kubwa kwetu kulitangaza bara
letu kupitia huduma zetu bora zinazotolewa katika ndege zetu.
Tumedhamiria kukuza vipaji vya wasanii wachanga barani Afrika.”
Bi.
Muhati aliongeza kwa kusema kuwa ushirikiano huo ni uthibitisho wazi
unaodhihirisha jinsi shirika hilo linavyojitolea katika kukuza fani ya
muziki barani Afrika, na pia utashi na mapenzi makubwa ya shirika hilo
kuona kuwa linakuwa sehemu ya kukuza vipaji na maendeleo ya wasanii wa
Afrika.
Mwanamuziki
ambaye ni mshindi wa tuzo ijulikanayo kama Grammy Award ambaye pia ni
mwandaaji wa muziki, Zwai Bala, magwiji wa Kwaito kutoka Afrika Kusini,
Kikundi cha TKZee, wataongoza maonyesho hayo ya muziki. Brett Lotriet,
ambaye ni mwandaaji na mwongozaji wa kimataifa wa maonyesho ya TV ni
miongoni mwa vinara ambaye ataoongoza uandaaji wa maonyesho ya Coke
Studio Msimu wa Tatu kadri matukio yatakavyokuwa yakitokea.
Wanamuziki
wakiwa pamoja na bendi za wasanii nyota wa ndani watatoa nyimbo mpya
kila wiki ambazo zitaandaliwa na waandaaji wa ndani na wale wa
kimataifa. Baadhi ya waandaaji ni pamoja na Jaaz Odongo, Eric Musyoka na
Kevin Provoke kutoka Kenya, Cobhams Asuquo, Masterkraft na Chopstix
kutoka Nigeria, Owour Arunga kutoka Marekani, Nahreel kutoka Tanzania na
Silvastone kutoka Uingereza. Yakiwa yamesheheni nyota wakali wa muziki,
maonyesho haya ya msimu huu yataufanya muziki wa Afrika ukue na kufikia
katika hatua mpya ya juu zaidi.
Kwa Mhariri:
Mash-up
ni wimbo au tungo ya muziki ambao umeandaliwa kwa kuchanganya nyimbo
mbili au zaidi zilizorekodiwa mapema, na kwa kawaida hufanywa kwa
kuchanganya nyimbo hizo ili kutoa kitu kipya kinachowajumuisha
wanamuziki wote wahusika katika nyimbo zilizochanywa.
Kwa
habari na taarifa zote kuhusu Coke Studio Africa ikiwa ni pamoja na
wasanii, lyrics & Television airing times tufuate kwa
#cokestudioafrica au online katika link zifuatazo:
No comments:
Post a Comment