Mkuu
wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi
na Utamaduni, Bi. Zulmira Rodrigues (katikati) akiambatana na Mbunge wa
viti maalum CCM, anayewakilisha watu wenye ulemavu, Mh. Al shaymaa
Kwegyir (kushoto) walipotembelea shule msingi Mitindo ya watoto wenye
ulemavu wa ngozi, macho na masikio iliyopo katika wilaya ya Misungwi nje
kidogo ya jiji la Mwanza. Kulia ni Mtaalamu wa Jinsia na Haki za
Binadamu kutoka UNESCO Tanzania, Bi. Annica Moore.
Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog)
Na Modewjiblog team
Mkuu wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO)Tanzania, Zulmira
Rodrigues amesisitiza umuhimu wa kuwapenda watoto wenye ulemavu wa
ngozi katika jamii baadala ya kuwatenga .
Zulmira
alisema hayo alipotembelea watoto wenye ulemavu wa ngozi katika shule
ya msingi ya Mitindo iliyopo katika wilaya ya Misungwi nje kidogo ya
jiji la Mwanza mwishoni mwa juma
Shule hiyo ya serikali ina wanafunzi zaidi ya 1000 wakimo wenye ulemavu 202 .
Kati
yao 81 ni wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi ambao wanahifadhiwa na
serikali katika shule hiyo maasa 24 kufuatia wimbi la mauaji la watu
wenye ulemavu wa ngozi katika mikoa ya kanda ya ziwa .
Hata
hivyo Mkuu wa ofisi na mwakilishi wa UNESCO Tanzania alionekana kupatwa
huzuni kubwa kutokana hali ya maisha ya watoto hao .
“
Nimehuzunika sana (I am so sad). Sio tabia ya watu wa Afrika kuwatenga
watu wanyonge (weak people)”alisema huku akitokwa na machozi mara baada
ya kuwatembelea watoto hao na kuongea nao pamoja na uongozi wa shule
hiyo.
Alisema
ni muhimu watoto hao wenye ulemavu wa ngozi kuwa wanavaa nguo za mikono
mirefu ili kuwakinga na jua kwa ajili ya kulinda afya zao.
Hata
hivyo Zulmira alipongeza jitihada zinazofanywa na serikali ya
Tanzania kulinda watu wenye ulemavu wa ngozi na kutoa wito kwa wadau
wote kuunga mkono juhudi hizo.
Mkuu
wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi
na Utamaduni, Bi. Zulmira Rodrigues akisaini kitabu cha wageni ofisini
kwa Mwalimu msingi Mitindo iliyopo katika wilaya ya Misungwi nje kidogo
ya jiji la Mwanza.
Katika
ziara hiyo, Zulmira alikuwa amefuatana na mbunge wa viti maalum
anayewakilisha watu wenye ulemavu wa ngozi (albinism) Mh. Al shaymaa
Kwegyir.
Mbunge
huyo pia alisema kitendo cha watoto wenye ulemavu wa ngozi kukosa
malezi na mapenzi ya wazazi ni changomoto kubwa iliyopo kwa sasa.
Alisema ni jukumu la watu wote kulinda na kusadia kuboresha maisha ya watu wenye ulemavu wa ngozi.
“Ufumbuzi wa matatizo ya wetu wenye ulemavu wa ngozi sio kazi ya serikali tu, ni jukumu la kila mtu”,mbunge huyo alisisitiza.
Aliahidi kuwasilisha bungeni baadhi ya changamoto zinazowakabili wanafunzi walemavu waliopo katika shule hiyo ya Mitindo.
Mwalimu
Mkuu wa shule hiyo Kurwa Ng’hwelo alisema serikali inatumia zaidi ya
shilingi milioni 10 kuwa ajili ya mahitaji ya chakula kwa wanafunzi wote
wenye ulemavu wapatao 202 kila mwezi.
Shule hiyo inakabiliwa na upungufu mkubwa wa watumishi wanaosadia wanafunzi hao walemavu.
Mwalimu
wa shule ya msingi Mitindo, Kulwa Ng'hwelo akitoa maelezo ya idadi ya
wanafunzi wenye ulemavu wanaosoma shuleni hapo ambao ni 202 huku 81
wakiwa na albinism kwa Mkuu wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja
wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, Bi. Zulmira Rodrigues
(kushoto) aliyetembelea shule hiyo kuangali changamoto zinazowakabili
watoto wenye ulemavu wa ngozi.
Mwalimu
wa shule ya msingi Mitindo, Kulwa Ng'hwelo akimwonyesha mazingira ya
eneo la shule hiyo Mkuu wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa
Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, Bi. Zulmira Rodrigues
aliyeambatana na Mbunge wa viti maalum CCM, anayewakilisha watu wenye
ulemavu, Mh. Al shaymaa Kwegyir.
Mkuu
wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi
na Utamaduni, Bi. Zulmira Rodrigues akisalimiana na baadhi ya wanafunzi
wa kutwa wanaosoma katika shule ya msingi Mitindo mara baada ya
kuwasili shuleni hapo akiwa ameambatana na Mbunge wa viti maalum CCM,
anayewakilisha watu wenye ulemavu, Mh. Al shaymaa Kwegyir.
Mkuu
wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi
na Utamaduni, Bi. Zulmira Rodrigues akizungumza na wanafunzi hao
waliofurahia ujio wake.
Pichani ni moja ya jengo lililojengwa na Ubalozi wa Japan nchini Tanzania.
Mmoja
wa watoto wenye ulemavu wa ngozi (Albinism) akitoka bwenini kuelekea
chumba maalum kwa ajili ya kujipatia chakula cha mchana katika shule ya
msingi Mitindo huku akionekana kutembea kwenye jua kali pasipo na kuwa
na nguo ndefu ya kufunika hadi mikononi kujikinga na mionzi ya jua
inayopelekea kupata saratani ya ngozi.
Mtoto
mwenye ulemavu wa ngozi (Albinism) ambaye jina lake halikuweza
kupatikana kiurahisi akila chakula cha machana huku akijikuna kutokana
na maumivu makali anayosikia ya majeraha ya mionzi ya jua iliyoharibu
mikono yake na kubadilika rangi ambayo athari yake baadae ni saratani ya
ngozi.
Na
hii ndio hali halisi ya binti huyu katika mikono yake kutokana na
kutembea kwenye jua bila kusitiri mikono yake na nguo ndefu.
Baadhi ya watoto wa bweni wenye Albinism wakijipatia chakula cha mchana jikoni.
Mtoto
mwingine aliyeathiriwa na mionzi ya jua miguuni na kupelekea kubadilika
rangi kuwa mwekundu kutokana na kukosa nguo ndefu za kujisitiri na
mionzi ya jua... wakiendelea kujinoma na chakula cha mchana.
Mkuu
wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi
na Utamaduni, Bi. Zulmira Rodrigues akionyesha uso wenye huzuni kubwa
kutokana na mazingira magumu waliyonayo watoto hao shuleni hapo. Kushoto
ni Mbunge wa viti maalum CCM, anayewakilisha watu wenye ulemavu, Mh. Al
shaymaa Kwegyir aliyeambatana na Bi. Zulmira Rodrigues kutembelea shule
hiyo. Katikati ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya msingi Mitindo, Kulwa
Ng'hwelo.
Mkuu
wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi
na Utamaduni, Bi. Zulmira Rodrigues (kulia) akisisitiza jambo kwa
Mwenyekiti wa kamati ya shule ya msingi Mitindo, Kalunde Cosmas
alipofanya ziara fupi ya kutembelea shule hiyo na kujionea changamoto
zinazowakibili watoto wenye ulemavu wa ngozi (Albinism).
Mbunge wa viti maalum CCM, anayewakilisha watu wenye ulemavu, Mh. Al shaymaa Kwegyir akimwonyesha mwandishi wa modewji blog (hayupo pichani) majeraha ya kuungua na jua kwa mmoja wa watoto mwenye albinism shuleni hapo.
Mkuu
wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi
na Utamaduni, Bi. Zulmira Rodrigues akizungumza jambo na mtoto mwenye
ulemavu wa ngozi aliyekuwa akijipatia chakula cha mchana.
Mdau
Semeni Kingaru akimsimamia kula chakula cha mchana mtoto mdogo kuliko
wote mwenye albinism aliyeonekana kukosa upendo wa wazazi wake kwa
kipindi kirefu na kufarijiwa na ugeni huo uliofika shuleni hapo.
Mbunge
wa viti maalum CCM,anayewakilisha watu wenye ulemavu, Mh. Al shaymaa
Kwegyir akibadilishana mawazo na mabinti wa shule ya msingi Mitindo
alipowatembelea na Bi. Zulmira Rodrigues.
Mkuu
wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi
na Utamaduni, Bi. Zulmira Rodrigues (kulia) akisaidiana na Mdau Semeni
Kingaru kugawa zawadi ya juisi kwa watoto wa shule ya msingi Mitindo.
Mtaalamu
wa Jinsia na Haki za Binadamu kutoka UNESCO, Bi. Annica Moore
aliyeambatana na Mkuu wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa
Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, Bi. Zulmira Rodrigues (hayupo
pichani) akifurahi jambo wakati akigawa zawadi ya juisi mmoja watoto
wenye albinism shuleni hapo.
Mkuu
wa ofisi na Mwakililishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshughulikia Elimu,Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira
Rodrigues akiendelea na zoezi la ugwaji zawadi ya juisi kwa watoto wenye
ulemavu wa ngozi, macho na masikio wa shule ya msingi Mitindo iliyopo
katika wilaya ya Misungwi nje kidogo ya jiji la Mwanza alipowatembelea
mwishoni mwa juma akiwa ameambata na Mbunge wa viti maalum
CCM,anayewakilisha watu wenye ulemavu, Mh. Al shaymaa Kwegyir (hayupo
pichani).
Baadhi ya watoto wenye ulemavu wa macho wakijumuika na wenzao wenye ulemavu wa ngozi na masikio kujipatia chakula cha mchana.
Mtoto mdogo kuliko wote mwenye albinism anayeonekana kukosa lishe bora inayostahili kutokana na umri wake ambapo modewjiblog imebaini kuwa mtoto huyu ana "Utapiamlo" kutokana na kukosa lishe hiyo bora. Dalili moja wapo ni tumbo lake kuwa kubwa na gumu.
Mkuu
wa ofisi na Mwakililishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu,
Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akimnywesha
juisi mtoto mdogo kuliko wote anayelelewa kwenye shule ya msingi Mitindo
ya watoto wenye uhitaji maalum ambao ni walemavu wa ngozi, macho na
masikio alipofanyia ziara fupi mwishoni mwa juma mkoani Mwanza.
Mkuu
wa ofisi na Mwakililishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu,
Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akimnyeshwa
juisi mtoto menye ulemavu wa macho alipotembelea shule ya msingi Mitindo
iliyopo wilaya ya Misungwi nje kidogo ya jiji la Mwanza.
Mkuu
wa ofisi na Mwakililishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu,
Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akiwa na uso
wa huzuni kutokana na mazingira ya watoto hao na kupelekea kumwaga
machozi kwa uchungu yeye kama mama mwenye kuthamini upendo. Kushoto ni
Mh. Al Shaymaa Kwegyir.
Bw.
Abdulaziz Mbegele wa kitengo cha Logistic kutoka UNESCO, akimnywesha
juisi mtoto mwenye ulemavu wa macho wakati wa ziara hiyo na Mkuu wa
ofisi na mwakilishi wa UNESCO nchini Tanzania.
Mtoto
alyefahamika kwa jina moja tu Kevin mwenye umri wa miaka 11 ambaye
alifikishwa kwenye shule hiyo akiwa mdogo sana na wazazi wake
kumtelekeza hadi leo huku akiwa hamjui mama, baba, mjomba, dada, kaka
wala shangazi..... kisa amezaliwa na albinism....!
Mtoto Kevin akipata "self" na mjomba wake mpya Zainul Mzige wa modewjiblog aliyeambatana na ugeni huo.
Mkuu
wa ofisi na Mwakililishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu,
Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akizungumza na
waandishi wa habari na kutoa hisia zake kuhusiana na changamoto
zinazowakabili watoto wenye ulemavu wa nguvu na kusisitiza upendo kwa
watu wenye albinism.
Mbunge
wa viti maalum CCM, anayewakilisha watu wenye ulemavu, Mh. Al shaymaa
Kwegyir akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani).
No comments:
Post a Comment