Matukio : Taswira ya Dk. Gharib Bilal Akimalizia Ziara yake ya Siku 3 , Nchini China - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Friday, 22 May 2015

Matukio : Taswira ya Dk. Gharib Bilal Akimalizia Ziara yake ya Siku 3 , Nchini China

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Makamu wa Rais wa China, Li Yuanchao, wakati alipowasili kwenye Ukumbi Maalum kwa watu wa China. 'Peoples Great Hall', jijini Beijing China kwa ajili ya mazungumzo rasmi, alipoalikwa kwenye chakula cha jioni na Makamu wa Rais wa China baada ya kumaliza ziara yake ya siku tatu nchini humo.  Mei 20, 2015.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya Viongozi wa Serikali ya China, wakati alipowasili kwenye ukumbu Maalum wa watu wa China, 'Peoples Great Hall' kwa ajili ya mazungumzo na Makamu wa Rais wa China, Li Yuanchao, baada ya kumaliza ziara yake ya siku tatu nchini humo, Mei 20, 2015.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, na mwenyeji wake Makamu wa Rais wa China, Li Yuanchao, wakisimama kwa heshima wakati zikipigwa nyimbo za Taifa la Tanzania na China, kwenye mapokezi yake katika Ukumbi Maalum wa Watu wa China, kwa ajili ya mazungumzo baada ya kumaliza ziara yake ya siku tatu nchini Nchina.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na mwenyeji wake Makamu wa Rais wa China, Li Yuanchao, wakati akikagua gwaride la heshima kwenye Ukumbi Maalum wa watu wa China, Peoples Great Hall, wakati alipofika kwa mazungumzo na mwenyeji wake baada ya kumaliza ziara yake ya siku tatu nchini humo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na ujumbe wake (kushoto) akiwa katika mazungumzo na Makamu wa Rais wa China, Li Yuanchao na ujumbe wake (kulia) kwenye Ukumbi maalum wa Watu wa China, 'Peoples Great Hall' baada ya kumaliza ziara yake ya siku tatu nchini China.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisindikizwa na mwenyeji wake, Makamu wa Rais wa China, Li Yuanchao, baada ya mazungumzo yao kwenye Ukumbi Maalum wa Watu wa China, jijini Beijing China. Kushoto ni mkarimani wa Makamu wa Rais wa China.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na mwenyeji wake Makamu wa Rais wa China, Li Yuanchao, baada ya mazungumzo yao kwenye Ukumbi Maalum wa Watu wa China, jijini Beijing China. Makamu wa Rais Dkt. Bilal, amemaliza ziara yake ya siku tatu nchini China. Picha na OMR

No comments:

Post a Comment