Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ni Mwenyekiti wa CCM Taifa
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Rais wa Msumbiji Mhe.Filipe
Jacinto Nyusi kwenye Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mjini
Dodoma.
Rais
wa Msumbiji Mhe.Filipe Jacinto Nyusi akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM
Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana mara baada ya kuwasili kwenye Makao
Makuu ya CCM mjini Dodoma.
Rais wa Msumbiji Mhe. Filipe Nyusi akisalimiana na wanachama na wapenzi wa CCM waliojitokeza kumpokea na kumkaribisha Dodoma.
Rais
wa Msumbiji Mhe.Filipe Jacinto Nyusi akivishwa skafu na vijana wa
Chipukizi wa CCM mkoa wa Dodoma wakati wa mapokezi kwenye Makao Makuu ya
Chama.
Baadhi
ya Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ,pamoja na viongozi wengine
wa CCM mkoa wa Dodoma wakiimba wakati wa kumkaribisha Rais wa Msumbiji
Mheshimiwa Filipe Nyusi kwenye makao makuu ya CCM mjini Dodoma.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akitoa neno la kumkaribisha Rais
wa Msumbiji na Mwenyekiti wa Chama cha Frelimo Mhe. Filipe Nyusi kwenye
makao makuu ya CCM mjini Dodoma.
Mwenyekiti
wa CCM Taifa ,Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza kabla ya
kumkaribisha Rais wa Msumbiji kuhutubia viongozi mbali mbali wa CCM
wakiwemo baadhi ya wajumbe wa Halmashauri Kuu
Mpigania
Ukombozi wa Msumbiji Mzee Aberto Chipande akizungumza kabla ya Rais
Filipe Nyusi kuhutubia wana CCM ambapo alielezea namna harakati za
kuikomboa nchi yao zilivyoanza, kupangwa na kuratibiwa Kongwa Dodoma na
kuanza safari ya kuelekea vitani mwaka 1963 na kusema Dodoma ni nyumbani
kwake.
Baadhi
ya wajumbe wa Halmashauri Kuu, Viongozi wa CCM mkoa wa Dodoma pamoja na
wageni waalikwa wakisikiliza hotuba ya Rais Filipe Nyusi kwenye ukumbi
wa NEC mjini Dodoma.
Rais wa Msumbiji Mhe. Filipe Nyusi akihutubia kwenye ukumbi wa NEC ,Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma.
Rais wa Msumbiji Mhe. Filipe Nyusi akijaribu kofia ya CCM ikiwa sehemu ya zawadi alizopewa na CCM.
Rais
wa Msumbiji Filipe Nyusi pamoja na Rais wa Tanzania Jakaya Mrisho
Kikwete wakiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa halmashauri Kuu ya
CCM Taifa mjini Dodoma
Rais
wa Msumbiji Mhe. Filipe Nyusi akiwaaga wana CCM mara baada ya
kuwahutubia ambapo alisisitiza kuwa Frelimo itaendelea kudumisha
mshikamano wao na CCM.
No comments:
Post a Comment