Matukio / Mgomo : Taswira ya hali ilivyokuwa katika Mgomo wa Madereva wa Mabasi ya Mikaoni, Ubungo Jijini Dar - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633


PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0676 643 633

Wednesday, 6 May 2015

Matukio / Mgomo : Taswira ya hali ilivyokuwa katika Mgomo wa Madereva wa Mabasi ya Mikaoni, Ubungo Jijini Dar

 Hali ilikuwa tete pale mawe yalipokuwa yakirushwa, na kupelekea baadhi ya viongozi pamoja na wanahabari waliokuwepo kwenye eneo hilo kukusanyika sehemu moja. hivyo polisi walilazimika kutumia mbinu zao na kufanikiwa kulituliza tukio hilo.
 Baadhi ya wanahabari wakinawa maji kufuaria moshi wa Mabomu ya Machoni yaliyokuwa yakipigwa Ubungo mchana.
 Baadhi ya Madereva na Makondakta wa Mabasi wanaondelea na Mgomo, wakiwa wamekaa juu ya Kontena zilizopo kwenye Kituo kikuu cha Mabasi, Ubungo jijini Dar es salaam kusubiria mustakabali wao, huku ulinzi Mkali wa Jeshi la Polisi ukiwa umetawala eneo hilo.
 Ghafla likazuka tukio la kurushwa mawe kutoka kwa watu wasiojulikana waliokuwa nje ya Stendi hiyo na kupeleke watu wote waliokuwa kwenye eneo hilo kukusanyika sehemu moja ili kujinusuru.
 
 Ulinzi ulitawala eneo lote la Ubungo leo.
 Baadhi ya Madereva na Makondakwa wao wakimzogoa mmoja wa Viongozi wao alikubali kuzungumza na Viongozi wa Serikali waliofika eneo hilo.
 Muda mfupi baadae, Aliwasili Mbunge wa Jimbo la Hai na Mwenyekiti wa CHADEMA, Mh. Freeman Mbowe ambaye alipokelewa kwa shangwe na Madereva hao.

Shangwe zikiendelea.
Mmoja wa viongozi wa Madereva akiwasihi wenzake kutulia ili kuwasikiliza viongozi waliokwenda kuwasiliza.

No comments:

Post a Comment