Bodi ya UTT-PID ikiongozwa na mwenyekiti wake Mrs. E Mlaki pamoja na
Menejimenti wakiwa na wenyeji wao katika jiji la Chengdu ambapo
walifanya ziara katika maeneo tofauti ya uwekezaji na manufaa wanayopata
wananchi wa jiji hilo. Ziara hiyo ya siku Tano katika Miji tofauti
inatarajia kukamilika Tarehe kumi kabla ya kurejea nyumbani.
Na Mwandishi Maalum
Bodi
ya Taasisi ya Miradi na Maendeleo ya Miundombinu iliyo chini ya Wizara
ya Fedha (UTT-PID), pamoja na Menejimenti yake ipo nchini China katika
ziara maalum ya Mafunzo na kujenga uzoefu ya siku tano ikiwa na lengo
la kuimmalisha utendaji kaziw wa taasisi hiyo.
Katika
ziara hiyo, Bodi ya UTT-PID, ikiongozwa na mwenyekiti wake Mrs. E
Mlaki pamoja na Menejimenti wapo katika miji mbalimbali na kutembelea
maeneo tofauti ya uwekezaji ilikushuhudia manufaa wanayopata wananchi
wa maeneo hayo.
Kazi za UTT-PID ni pamoja na Utoaji huduma za ushahuri katika maeneo
ya upembuzi yakinifu wa miradi mbalimbali, Uratibu wa fedha na huduma
zinazohusiana katika maandalizi ya mapendekezo ya miradi kwa benki au
taasisi za fedha, uteuzi wa watoa huduma kuhusiana na maandalizi ya
zabuni na usimamizi wa majengo na mali ambao ni utoaji wa huduma fanisi
za usimamizi wa majengo yaliyochini ya uangalizi thabiti wa taasisi.
Bodi ya UTT-PID pamoja na Menejimenti ikipata Maelezo kutoka wataalum wa uzalishaji nishati toka mji wa Chengdu.
Pichani Wajumbe wa Bodi ya UTT-PID wakiwa na wenyeji wao ndani ya ukumbi wa mikutano nchini China katika ziara hiyo ya siku 5.
Wajumbe wa Bodi ya UTT-PID wakiwa na wenyeji wao ndani ya ukumbi wa mikutano nchini China katika ziara hiyo ya siku 5.
Mkutano
ukiendelea baina ya Wajumbe wa Bodi ya UTT-PID wakiwa na wenyeji wao
ndani ya ukumbi wa mikutano nchini China katika ziara hiyo ya siku 5.
Bodi
ya UTT-PID ikiongozwa na mwenyekiti wake Mrs. Elpina Mlaki (wa pili
kushoto) pamoja na Menejimenti wakiwa na wenyeji wao katika jiji la
Chengdu ambapo walifanya ziara katika maeneo tofauti ya uwekezaji na
manufaa wanayopata wananchi wa jiji hilo.
Wajumbe wa Bodi ya UTT-PID, wakipata maelezo kutoka kwa mtaalamu kutoka
Zipingpu Hydropower mwenyeji wao, jinsi gani uzalishaji unavyofanyika
na usambazaji wa nguvu za nishati. Mjumbe wa Bodi Mrs. J Mmari (kulia),
akifuatiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo Dr. Gration Kamugisha
mwenye shati jeupe na kushoto ni Mwanasheria wa Taasisi hiyo, Bi. Tuzo
Mpiluka.
No comments:
Post a Comment