
Mwakilishi
wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania { RED CROSS }
Bwana Shaaban Ali Iddi akikabidhi msaada wa Viatu Pair 90 kwa Katibu wa
Kamati ya Taifa ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar Dr. Khalid Salum Moh’d
kwa ajili ya watoto wa familia zilizopata maafa ambao wapo Kambini
Skuli ya mwanakwerekwe “C”.

Katibu
wa Kamati ya Taifa ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar Dr. Khalid Salum
Moh’d akiushukuru Uongozi wa Red Cross kwa misaada yao ya Kibinaadamu
waliyotoa kwa ajili ya familia zilizopatwa na maafa wiki iliyopita.

Uongozi
wa Chama cha Msalaba mwekundu Tanzania ukimsikiliza Katibu wa Kamati ya
Taifa ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar Dr. Khalid Salum Moh’d hayupo
pichani akitoa nasaha zake baada ya kupokea msaada uliotolewa na Uongozi
huo.
Chama
cha Msalaba mwekundu Tanzania { red Cross } kimekabidhi msaada wa viatu
Pair 90 kwa ajili ya watoto wa familia zilizowekwa Kambini katika
Skuli ya Sekondari ya Mwanakwerekwe “C” baada ya Nyumba zao kujaa maji
ya mvua.
Msaada
huo umefuatia Mvua za Masika zilizotokea usiku wa kuamkia Tarehe 3 Mei
mwaka huu na kuleta maafa makubwa yaliyosababisha zaidi ya Nyumba 700
kuathirika ndani ya Mkoa wa Mjini Magharibi na kuzikosesha makaazi
Familia zilizokuwa zikiishi katika nyumba hizo.
Ujumbe
wa Red Cross Mkoa wa Mjini Magharibi ukiongozwa na Mwakilishi wa
Mkutano Mkuu wa Chama hicho Bwana Shaaban Ali Iddi umekabidhiwa msaada
huo kwa Katibu wa Kamati ya Taifa ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar
ambae pia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Dr. Khalid Salim Moh’d hapo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Akizungumza
katika hafla hiyo fupi Bwana Shaaban Ali Iddi alisema Uongozi wa Red
Cross ulifikia hatua ya kutoa msaada huo baada ya kugundua kwamba idadi
kubwa ya watu waliohifadhiwa kwenye kambi ya dharura ya Mwanakwerekwe
“C” ni Watoto wadogo.
Alisema
Red Cross imeguswa na tukio hilo la mafuriko hivyo licha ya juhudi
wanazochukuwa za kutoa misaada mbali mbali ya huduma lakini pia
ikawajibika kuongeza msaada huo wa Viatu ambao kwa kiasi kikubwa
utawasaidia watoto hao.
Mwakilishi
huyo wa Mkutano Mkuu wa Red Cross Taifa aliyaomba Mashirika na Taasisi
nyengine za Kitaifa na Kimataifa kuendelea kuguswa na Tukio hilo na
kutoa misaada kwa jukumu hilo si vyema ikaachiwa pekee Serikali Kuu.
Akipokea
Msaada huo Katibu wa Kamatio ya Taifa ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar
ambae pia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rsis wa Zanzibar
Dr. Khalid Salum Moh’d aliipongeza Red Cross kwa jitihada zake
inazoendelea kuchukuwa katika kusaidia huduma za Kijamii.
Dr.
Khalid alisema Viongozi na Wanachama wa Chama cha Msalaba Mwekundu
Tanzania muda wote wamekuwa karibu na Serikali hasa wakati yanapotokea
matukio ya majanga na maafa.
Katibu
huyo wa Kamati ya Taifa ya kukabiliana na Maafa Zanzibar aliupongeza
Uongozi wa Red Cross kwa hatua yake hiyo ambayo itasaidia kupunguza
machungu ya Watoto hao, wengi kati yao wamepoteza vitu vyao vyote
zikiwemo nguo na hata madaftari ya Skuli.
Alisema
Kambi ya dharura ya Mwanakwerekwe “ C “ hivi sasa ina zaidi ya watoto
74 walio chini ya umri wa miaka 14 wanaoendelea kuhifadhiwa ambao
watafaidika na msaada huo wa viatu.
“
Asilimia kubwa ya Watoto hao waliopo Kambini wamepoteza Vitu vingi
ikiwemo Madaftari ya Skuli, Nguo, Viatu na vitu vyengine muhimu
wanavyotumia ambavyo vingi kati yao tayari Idara ya Maafa kupitia
Taasisi na Mshirika hisani wameshapatiwa “. Alifafanua Da. Khalid Salum
Moh’d.
Pia
aliyashukuru na kuyapongeza Mashirika na Taasisi za Umma na hata zile
Binafsi zilizojitolea kutoa misaada mbali mbali ya Kibinaadamu na
kuziomba zisichoke kwa vile bado mahitaji zaidi kwa waathirika hao
yanahitajika.
Katibu
huyo wa Kamati ya Taifa ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar alieleza
kwamba Serikali imeandaa mpango maalum wa usafiri kwa watoto wote
waliopo Kwenye Kambi ya dharura Mwanakwerekwe “C” kuendelea na masomo
yao kwenye skuli mbali mbali wanazotoka.
No comments:
Post a Comment