Mkurugenzi
wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akizungumza
kuashiria uzinduzi rasmi wa kituo cha huduma kwa wateja cha
Shirika hilo uliofanyika kwenye ukumbi wa Kituo hicho kilichopo Makao
makuu ya Shirika barabara ya Ufukoni na Ali Hassan Mwinyi, jijini Dar es
salaam, Kulia kwake ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa
Jamii, Susan Omari.
Pichani ni baadhi ya waandishi wa habari wanaoshuhudia tukio hilo .
Maofisa
wa Shirika la Nyumba wanaokiendesha kituo hicho kipya cha huduma kwa
Wateja wakiwa kazini mara baada ya kuzinduliwa, timu ya kituo hicho
inaongozwa na mwanahabari Mzoefu Domina Rwemanyila.
Mkurugenzi
waShirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akizungumza

salaam, Kulia kwake ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma na
Huduma kwa Jamii, Susan Omari.
Maofisa
wa Shirika la Nyumba wanaokiendesha kituo hicho kipya cha huduma kwa
Wateja wakiwa kazini mara baada ya kuzinduliwa, timu ya kituo hicho
inaongozwa na mwanahabari Mzoefu Domina Rwemanyila.
Maofisa
wa Shirika la Nyumba wanaokiendesha kituo hicho kipya cha huduma kwa
Wateja wakiwa kazini mara baada ya kuzinduliwa, timu ya kituo hicho
inaongozwa na mwanahabari Mzoefu Domina Rwemanyila.
Wakurugenzi wa Shirika hilo wakishuhudia tukio la kuzinduliwa kwa tukio hilo
Pichani ni baadhi ya waandishi wa habari wanaoshuhudia tukio hilo .
Picha zaidi za tukio la uzinduzi huu tutawaleteeni baadaye.
&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&
SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU UZINDUZI WA KITUO CHA HUDUMA KWA WATEJA
KWA NJIA YA SIMU NA MALIPO YA KODI KWA MFUMO WA SIMU ZA KIGANJANI – MEI
19, 2015
.................................................................................................
Katika
jitihada za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kuboresha huduma kwa
wateja kama ilivyoainishwa kwenye Mkataba wa Huduma kwa Mteja, leo
Shirika la Nyumba la Taifa linazindua huduma mbili, ambazo ni kituo cha
huduma kwa wateja na pili ni mfumo wa kulipa kodi za nyumba kwa kutumia
simu ya kiganjani.
Kituo
cha huduma kwa wateja kwa njia ya simu kitatumika kuhudumia wateja wetu
wote kwa kupiga simu pale wanapohitaji kufahamu juu ya huduma zetu na
bidhaa mbalimbali pamoja na kutoa taarifa mbalimbali za shirika
zinazohusu huduma kwenye makazi yao.
Wateja wataweza kupata huduma hii kupitia nambari +255 784 105 200 na
+ 255 222 162 800. Kupitia kituo hiki Shirika linawaahidi kwamba
maulizo na taarifa zozote zitakazoripotiwa zitapewa kipaumbele kwa
kupatiwa ufumbuzi haraka iwezekanavyo.
Katika
kuendelea kuboresha mfumo wa ukusanyaji kodi kutoka kwa wapangaji wetu,
Shirika limeanzisha mfumo wa kulipa kodi kupitia simu za kiganjani ili
wapangaji waweze kufanya malipo ya kodi zao bila ya usumbufu wowote
kupitia tigopesa, mpesa na airtel money.
Kupitia
mfumo huu, wapangaji wataweza kufanya malipo kwa kutumia simu zao na
wataweza kuhamisha fedha kutoka kwenye benki akaunti zao na kwenda
Shirika la Nyumba mahali popote walipo na kwa muda wowote ambao ni
muafaka kwao bila ya kufika katika vituo vyetu vya makusanyo ya kodi.
No comments:
Post a Comment