Sheria / Mtandaoni : Uchambuzi wa Sheria za Makosa Mtandao, 2015 - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


2 Apr 2015

Sheria / Mtandaoni : Uchambuzi wa Sheria za Makosa Mtandao, 2015

Awali ya yote nirudie kutoa pongezi kwa serikali kwa hatua hii muhimu waliyofikia ya kuwasilisha mswada wa sheria mtandao ambao naimani kubwa itakua na majibu mazuri ya kudhibiti na kuhimili vishindo vya uhalifu mtandao nchini. Naomba itambulike Tanznaia si ya kwanza kuwa na sheria za usalama mitandao na ukweli ni kwamba tumechelewa kwa kiasi Fulani. Nchi nyingi tayari zinasheria za usalama mitandao na zimeendelea kuboreshwa kadri teknolojia inavyo endelea kukua na kubadilika.

Nitaanza na mifano michache kunasheria mitandao zilizopendekeza kifungo cha maisha kwa wahalifu mtandao nchini Uingereza. Na katika Kikao cha usalama mitandao kilichopita mshiriki aliyekua nami meza kuu katika kuongoza moja ya kikao aliyetokea “US Secret service” alipata kuainisha adhabu ya miaka kumi na sita bado imeonekana ni ndogo na inashauriwa kuongezwa makali.

Aidha, Nieleze ushauri wa kuhakiki sheria mitandao zinaboreshwa na kuwa kali zaidi ni kutokana na athari ya uhalifu mtandao kua kubwa sana na imekua ikimgusa kila mmoja wetu – Kwan nje ya nchi kila siku tumekua tukipata habari mpya ya matukio ya kiuhalifu mtandao ambapo maelfu wamekua wakipoteza maisha, fedha na pia ufaragha wao umekua ukitumiwa vibaya na wahalifu mtandao.

Tanzania pia hatuko salama – Nimekua nikipata malalamiko mengi ya watu kudukuliwa faragha zao, kuibiwa fedha nyingi sana na wengine kufikia hata kujitoa maisha kwa kudalilisha mitandaoni.

Hayo yote yamekua yakisukuma wataalam usalama mitandao kuumiza vichwa kuhakiki wanakuja na mwarubaini wa uhalifu huu mtandao unaozidi kuota mbawa kila kukicha. Hapo ndipo mengi yakawekwa sawa katika kukabiliana na hali hii ikiwa ni pamoja na kukuza uelewa kwa watumiaji mtandao (Matumizi salama ya mitandao), Kuzalisha na kuongezea uwezo kwa wataalam wa usalama mitandao, kuwa na sharia stahiki za uhalifu mitandao, kukuza ushirikiano kutokana na uhalifu huu kutokua na mipaka, kuhimiza kupatikana kwa takwimu sahihi za uhalifu mitandao ili kuweza kutambua maeneo athirika zaidi.

Kwenye hili la Sheria ni hatua nzuri sana ambapo Tanzania imefikia ili kuweza kurahisisha mapambano dhidi ya uhalifu mtandao nchini na kuhakiki taifa linabaki salama kimtandao. Naimani Kila mmoja wetu ukizingatia wote ni wahanga kwa namna moja au nyingine ya uhalifu mtandao lazima tufurahie na kulipokea hili kwa mikono miwili. Wataalam wa usalama mitandao wamefurahishwa sana na hatua hii yetu na pongezi ni nyingi sana hadi sasa.

Kuondoa hofu Watanzania naomba nieleze kwamba katika kuandaa muswada huu wataalam na wadau mbali mbali walishirikishwa na badae kuvuka mipaka kwa wataalam kutoka mataifa mbali mbali katika maswala haya ya usalama mitandao kutoa maoni yao na kuboresha – Haikukomea hapo imepitia hatua kadhaa na hata kupelekea kauli yangu niliyo itoa katika moja ya vikao vya wataalam wa usalama mitandao kueleza kuwa “ Hatua za kitaalam zimekwisha sasa ipo kwenye hatua za kisiasa kuweza kupatiwa Baraka kabla ya kuwasilishwa bungeni” – Kauli ambayo wataalam
waliona taifa letu linachelewa sana kwani sharia zilikua hazina shaka na hata kupitiwa kwakwe kulipaswa kua kwa muda mfupi.

Nimepata kufatilia kwa karibu kinachozungumzwa na wengi, Hofu kubwa nilizo ziona ambazo nimeona nizitole ufafanuzi ni kama ifuatavyo: -


MOJA, hofu kuwa uchunguzi wa makosa haya inaweza ikawa inakiuka faragha. Naomba nieleze kuna anaefahamu faragha yake iko dhaifu kiasi gani mara tu anavyo kua mtandaoni? Ni wazi kabisa unapaswa kujua faragha haiingi matatani tu kwa sababu ya sharia hizi mtandao.

Uchunguzi wowote wa uhalifu mitandao duniani kote unahusisha uangalizi wa kina hatua kwa hatua kwa kila ushaidi wa kielektroniki ikiwa ni pamoja na kupitia kwa karibu kila chembe ya shaka ya kile kinachoweza kuonekana kinaweza kuwa na chembe ya sababu ya uhalifu mtandao.
KWA HABARI ZAIDI BOFYA HAPA >>>

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad