Muziki : SKYLIGHT BAND Yazidi Kuwapagawisha Mashabiki wake,njoo leo uone Vitu vipya - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Friday, 24 April 2015

Muziki : SKYLIGHT BAND Yazidi Kuwapagawisha Mashabiki wake,njoo leo uone Vitu vipya


Meneja wa Skylight Band Aneth Kushaba AK 47 akiimba mmoja ya nyimbo yenye hisia kali sambamba na msanii mwenzake Sam Mapenzi kwenye kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar
Sony Masamba akiendelea kutoa burudani huku akisindikizwa na wanamziki wenzake ambao ni Aneth Kushaba(wa pili kutoka kulia) pamoja na Sam Mapenzi(Kulia)
Ashura Kitenge akiimba kwa pamoja na Sam Mapenzi mbele ya mashabiki wa Skylight Band(hawapo pichani) kwenye kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar
Sam Mapenzi akitoa burudani huku akisindikizwa na wanamziki wenzake ambao ni Joniko Flower(wa kwanza kushoto), Ashura Kitenge(wa pili kutoka kulia) pamoja na Sony Masamba.
Aneth Kushaba AK 47 (kushoto) akiimba sambamba na Sony Masamba mbele ya mashabiki wao (hawapo pichani) kwenye kiota cha Thai Village, Masaki jijini Dar.
Meneja wa Skylight Band Aneth Kushaba AK 47 akiwaimbia mashabiki wa bendi hiyo waliofika kwenye Kiota Cha Thai Village kuburusika na Bendi hiyo.
Waimbaji wa Skylight Band wakizirudi ngoma kwenye kiota cha Thai Village
Msanii wa Skylight Band, Ashura Kitenge akicheza sambamba na mpiga jitaa
Sony Masamba akiimba kwa hisia ndani ya Kiota cha Thai Village
Waimbaji wa Skylight Band wakiendelea kutoa burudani kwa wapenzi na mashabiki wa bendi hiyo (hawapo pichani).
DSC_0353
Ni happy kwa mashabikiwa wa Skylight Band maana ni full kujiachia ndani ya Kiota cha Thai Village, Masaki jijini Dar.
Rapa mkongwe kwenye muziki wa Live Joniko Flower(wa kwanza kushoto) akiongoza kikosi cha bend ya Skylight waliokuwa wakitoa burudani kwa mashabiki wao (hawapo picha) kwenye kiota cha Thai Village, Masaki jijini Dar.
Ulifika ule muda wa kusugua mpaka utakate hii ni moja ya Style ya Bend ya Skylight waliyowafundisha mashabiki wa bend hiyo
NI mwendo sasa wa mduara mambo ya mwambo nayo yanahusika ndani ya Bendi ya Skylight njoo leo ujionee mambo yenyewe
Msanii wa Bendi ya Skylight, Aneth Kushaba(Kushoto) akicheza na mmoja wa mashabiki wakubwa wa bend hiyo
Mashabiki wa Bend ya Skylight wakiendelea kuserebuka kwenye Kiota Cha Thai Village, Masaki Jijini Dar
Sony Masamba ambaye ni mmoja wa waimbaji wa Skylight akiendelea kutoa burudani huku akisindikizwa na waimbaji wenzake.
Hii ni moja ya Kadi ya Member inatayotumika mpaka tarehe 31 mwezi wa 12 mwaka 2015
Mashabiki wa Skylight Band walioingia kwenye tano bora wakiendelea kucheza ili kuwapata watatu bora zaidi.
Joniko Flower (wa kwanza kushoto) pamoja na Sony Masamba(wa kwanza kulia) wakiendelea kuwashindanisha mashabiki wa Skylight Band walioingia kwenye nne bora ili kupata watu watatu watakaokabidhiwa Kadi za umember watakazokuwa wanazitumia kila siku ya Ijumaa ndani ya Kiota cha Thai Village
Washindi waliojinyakulia kadi za umember wa Skylight Band wakizirudi kwa furaha kwenye kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar
Mmoja wa washindi akicheza mara baada ya kupewa kadi ya Member wa Skylight na msanii wa bend ya Skylight Sam Mapenzi atakayokuwa anaitumia kila ijumaa ndani aya Thai Village jijini Dar
Mmoja wa washindi akikabidhiwa kadi ya member wa Skylight na msanii wa bend ya Skylight Sam Mapenzi mara baada ya kushinda .
Sam Mapenzi akizungumza jambo mara baada ya kumkabidhi shabiki wa bend ya Skylight kadi ya member atakayokuwa anaitumia kila ijumaa mpaka tarehe 31/12/2015.

No comments:

Post a Comment