TAARIFA YA JESHI LA POLISI KANDA MAALUM YA DAR ES SALAAM
JUU YA KUTIWA MBARONI KWA WATUHUMIWA SUGU WA KUPORA RAIA WA KIGENI NA
AKINA MAMA
Watuhumiwa wanne wamekamatwa jijini Dar es Salaam katika
makutano ya barabara ya Bibi Titi na Ohio karibu na Hotel ya Serena
baada ya kumpora raia wa kigeni wakiwa na gari dogo rangi ya kijivu
yenye nambari za usajili T787 DBU Toyota Cienta.
Hivi karibuni kumeibuka wimbi la wahalifu kuwapora pesa na
vitu vya thamani kama mikufu, bangili, hereni pia pete na vitu
mbalimbali vya thamani raia wa kigeni na akina mama ambao hupenda
kutembea na pochi. Wahalifu hawa hutumia gari dogo ambalo mara kwa mara
hubadilishwa namba zake za usajili na wakati mwingine gari hili
wanalitumia kama Tax bubu.
Leo tarehe 21/04/2015 majira ya saa 09:00 asubuhi katika
eneo la Posta Mpya watuhumiwa hawa walimdangavya bwana CEES S/O JAN
CONIJN, Miaka 27, raia wa Uholanzi aliyetaka kufika Klabu ya Leaders
kwamba wangempeleka eneo hilo kwa kutumia gari tajwa hapo juu. Baada ya
kuondoka na dereva kila baada ya mita 200 dereva huyo alikuwa
anasimamisha gari na kuongeza mtu mwingine kama abiria hadi walipotimia
wote wane.
Walimpeleka hadi maeneo ya Kinondoni kwa Manyanya na
walipofika eneo hilo walimweleza wazi kuwa wao ni wahalifu na walimtaka
awapatie pesa vinginevyo wangemuua. Aliwapatia pesa zote alizokuwa nazo
Tshs 75,000/= lakini hawakuridhika ndipo walipomtaka awapatie kadi ya
benki (ATM CARD) na nambari za siri (Pass Word).
Baada ya tukio hilo wakamtupa karibu na Hospitali ya
Mwananyamala na wao wakageuza gari kurudi katikati ya mji. Wakati tukio
hilo linatokea raia wema walishuhudia na kutoa taarifa kwa Polisi.
Polisi walifuatilia haraka na kuweka mtego uliowanasa watuhumiwa wote
katika eneo la makutano ya barabara ya Bibi Titi na Ohio karibu na Hotel
ya Serena.
Majina ya watuhumiwa waliokamatwa ni:
1. SALUM S/O SAID MTUMWA @ MARO, Miaka 25, Mkazi wa Chang’ombe Bora.
2. ALEX S/O INNOCENT MANGUKA @ MAKA, Miaka 30, Mkazi wa Kimara Temboni.
3. MOHAMED S/O ALLY ABDALLA @ MEDY, Miaka 27, Mkazi wa Mwananyamala.
4. STEPHANO S/O ALBERT KIKINDI @ KING, Miaka 32, Mkazi wa Mwananyamala.
1. SALUM S/O SAID MTUMWA @ MARO, Miaka 25, Mkazi wa Chang’ombe Bora.
2. ALEX S/O INNOCENT MANGUKA @ MAKA, Miaka 30, Mkazi wa Kimara Temboni.
3. MOHAMED S/O ALLY ABDALLA @ MEDY, Miaka 27, Mkazi wa Mwananyamala.
4. STEPHANO S/O ALBERT KIKINDI @ KING, Miaka 32, Mkazi wa Mwananyamala.
Walipopekuliwa watuhumiwa hawa walikutwa na simu
mbalimbali za mkononi zipatazo 11 ambazo zinachunguzwa kuhusiana na
mbinu ya uhalifu wanaoutumia. Pia ilikamatwa ATM CARD iliyochukuliwa kwa
mlalamikaji kabla watuhumiwa hao hawajaitumia. Aidha gari namba T787
DBU Toyota Cienta linashikiliwa kwa uchunguzi zaidi.
Miongoni mwa watuhumiwa waliokamatwa, wawili ambao ni
MOHAMED S/O ALLY ABDALLA @ MEDY, na STEPHANO S/O ALBERT KIKINDI @ KING,
tayari wanazo kesi nyingine mahakamani na wako nje kwa dhamana.
Sambamba na tukio hili oparesheni ya kuwakamata wahalifu
wengine wenye mtindo huu wa kuwapora wageni au wakina mama wenye mikoba
inaendelea na tunawaomba wananchi waonyeshe ushirikiano wa kutosha ili
kutokomeza vitendo hivyo viovu. Aidha hakuna silaha yoyote iliyotumika
au kukamatwa kama ilivyoripotiwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii.
S. H. KOVA,
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM,
DAR ES SALAAM.
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM,
DAR ES SALAAM.
No comments:
Post a Comment