Matukio : Huzuni Yatanda Wakati wa kutoa Heshima za mwisho kwa Bibi Mkwe wake Nape Nnauye - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Thursday, 23 April 2015

Matukio : Huzuni Yatanda Wakati wa kutoa Heshima za mwisho kwa Bibi Mkwe wake Nape Nnauye


 Jeneza lililobeba mwili wa marehemu Magdalena Petro Magige likiteremshwa kutoka kwenye gari tayari kwa kutoa heshima ya mwisho kabla ya safari ya kwenda kuupumzisha kijiji cha Kamange,Tarime mkani Mara.

 Ndugu , Jamaa na marafiki waliojitokeza kuja kutoa heshima za mwisho kwa mpendwa wao Bibi Magdalena Petro Magige aliyefariki  tarehe 19 Aprili jijini Dar es Salaam.
 Padri Valence Matungwa akitoa somo wakati wa misa maalum ya kumuaga marehemu Magdalena Petro Magige,Mikocheni jijini Dar es Salaam.
 Padri Ladislaus Kapinga akiongiza ibada wakati wa kumuaga marehemu Magdalena Petro Magige
 Mtoto wa Marehemu Norah P. Mukami akipokea ekaristi takatifu wakati wa misa maalumu ya kumuaga Magdalena Petro Mukami.

 Ndugu na jamaa waliojitokeza kwa wingi kwenye kutoa heshima ya mwisho kwa marehemu Magdalena Petro Magige.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza jambo na Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma Alhaji Adam Kimbisa na Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) mstaafu, Jenerali George Mwita Waitara wakati wa kutoa heshima za mwisho kwa marehemu Magdalena Petro Magige.

No comments:

Post a Comment