Mbunge
wa Jimbo la Kikwajuni na Mlezi wa Jumuiya ya Tanzania Yuoth Icon (TAYI)
Mhe.Eng Hamadi Yussuf Masauni akikabidhiwa Cheti cha Mchango wake kwa
Vijana kuhusiana na Amani kutoka kwa Mratibu wa UNESCO kwa Vijana
Tanzania Ndg Simba Mwinyi Simba kwa kutambua mchango wake kwa Vijana
Zanzibar kudumisha amani, hafla hiyo mefanyika katika Kituo cha Vijana
cha TAYI muembemadema Zanzibar
Mhe.Eng Hamad Masauni akionesha Cheti baada ya kukabidhiwa wakati wa Kongamano la Vijana wa TAYI .
Naibu
Katibu wa Vijana wa Umoja wa Mataifa Tanzania(YUNA) Bi, Pili Khamis,
akikabidhi Cheti kilichotolewa na YUNA kwa kuthamini Mchango wake kwa
Vijana Zanzibar Mhe.Eng Hamad Yussuf Masauni, makabidhiano hayo
yamefanyika katika jengo la Ofisi za TAYI muembemadema Zanzibar kushoto
Mratibu wa YUNA Zanzibar Ndg Ali Hemed.
Mhe.Eng. Masauni akioneshga Cheti chake baada ya kukabidhia kilichotolewa na YUNA kujali mchango wake kwa Vijana Zanzibar.
Vijana
wa Kituo cha TAYI wakifuatilia hafla hiyo ya makambidhiano ilioendana
na Kongamano la Vijana kuhusiana na Amani Zanzibar wakati wote,
Kongamano hilo limetayarishwa na Unesco kwa kushirikiana na Jumuiya ya
TAYI.
Mhe
Eng.Hamad Yussuf Masauni, akizungumza na Vijana wakati wa hafla ya
kukabidhiwa Vyeti ilioendana na Kongamano la Vijana kuhusiana na Amani
Zanzibar lililowashirikisha vijana wa TAYI na wa Vyuo Vikuu Zanzibar
lililofanyika katika Kituo cha TAYI Muembemadema Zanzibar na kudhaminiwa
Unesco.
Mratibu
wa Unesco Tanzania kwa Vijana Ndg Simba Mwinyi Simba akizungumza wakati
wa Kongamano hilo la Mafunzo ya kudumisha Amani kwa Vijana Tanzania
lililofanyika katika kituo cha Vijana cha TAYI muembemadema Zanzibar na
kushirikisha Vijana kutoka Vyuo Vikuu Zanzibar na Mabalozi wa Vijana wa
Amani.
Mratibu wa YUNA Ndg Ali Hemeid akizungumza na kutowa mafunzo kwa Vijana walioshiriki Kongamano hilo.
No comments:
Post a Comment