Mjumbe
wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif Ali Iddi
akizungumza katika mkutano wa ujirani mwema kati ya Kata ya Mtoni Wilaya
ya Temeka na Wilaya ya Dimani hapo Tawi la CCM Kwerekwe B.
Mkuu
wa Msafara wa Ujumbe wa Kata ya Mtoni Wilaya ya Temeke Mkoa wa Dar es
salaam Nd.Said Kabuma akitoa shukrani kwa mapokezi mazuri waliyopewa na
wenyeji wao Wilaya ya Dimani wakati wa kuagana baada ya kumaliza ziara
yao ya ujirani mwema Zanzibar.
Baadhi
ya Viongozi na wanachama wa ujirani mwema kati ya Kata ta Mtoni Wilaya
ya Temeka mkoa wa Dar es salaam na Wilaya ya Dimani Mkoa wa Magharibi
Zanzibar.
Mwenyekiti
wa Serikali ya Mtaa wa Mtoni ambae pia ni Katibu Mwenezi wa Kata hiyo
Wilaya ya bTemeke Mkoa wa Dar es salaam Ndugu Hija Makamba akielezea
mafanikio yanayopatikana kutoka na ujirani mwema kati ya pande hizo
mbili.
Balozi
Seiuf akimfariji na kumpa Pole Bibi Khadija Said Hassan wa Kata ya
Mtoni Wilaya ya Temeke ambaye alipata ajali ya kugongwa na vespa wakati
wa ziara yake ya ujirani mwema Zanzibar.
Picha na –OMPR – ZNZ.
Mjumbe
wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif Ali Iddi
alisema kwamba Watanzania Bara na Zanzibar wataendelea kushirikiana kwa
karne kadhaa zijazo kutokana na muingiliano wao wa kidamu uliopo kati
ya pande hizo mbili.
Alisema
uwepo wa ushirikiano huo ndio njia pekee itakayotowa fursa kwa
Watanzania hao kusaidiana katika kutatua changamoto zinazojichomoza
miongoni mwao na vizazi vyao.
Balozi
Seif Ali Iddi ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema
hayo wakati akizungumza katika mkutano wa ujirani mwema kati ya
Wanachama na Viongozi wa Mkoa wa Magharibi na wageni wao kutoka Kata ya
Mtoni Wilaya ya Temeke Mkoa wa Dar es salaam.
Mkutano
huo uliofanyika katika Tawi la Chama cha Mapinduzi Kwerekwe “B”
unafuatia ziara za ujirani mwema kati ya pande hizo mbili zinazofanyika
mwanzoni mwa mwezi wa Aprili ya kila mwaka kutegemea upande unaokuwa
mwenyeji wa ugeni huo.
Balozi
Seif alisema hakuna kikundi wala mtu anayeweza kuung’oa Muungano uliopo
wa Tanganyika na Zanzibar kutokana na historia yake kwa jinsi
ulivyoimarika kwa miaka kadhaa iliyopita.
Amewataka
na kuwaomba Watanzania wote kuiunga mkono Katiba iliyopendekezwa na
Bunge Maalum la Katiba kwa vile inakidhi mahitaji na haki za makundi
yote yaliyopo hapa Nchini.
Balozi
Seif alifahamisha kwamba Katiba iliyopendekezwa yenye muundo wa mfumo
wa Serikali mbili ndio itakayolivua Taifa la Tanzania kuendelea kudumu
kwa zaidi ya miaka mengine hamsini ijayo.
Akizungumzia
suala la Uchaguzi Mkuu wa mwezi Oktoba mwaka huu Mjumbe huyo wa Kamati
Kuu ya CCM Taifa aliwataka Wanachama wa CCM Kuheshimu maamuzi ya Vikao
vya Chama chao wakati vinapofanya kazi ya kuteuwa wagombea wao.
Alisema
ni vyema kwa wanachama hao kukubali maamuzi yanayotolewa na chama chao
kwa kuwaunga mkono wagombea waliopendekezwa katika ngazi zote kuingia
kwenye kinyang’anyiro cha uchaguzi mkuu ujao.
Akisoma
risala Katibu wa Kamati ya ujirani mwema Ndugu Muhidini Makame Ussi
alisema ujirani mwema kati ya Kata ya Mtoni Wilaya ya Temeke na Wilaya
ya Dimani umeanza tokea mwaka 1995.
Nd.
Muhidini alisema ujirani mwema huo unaojumuisha Viongozi na wanachama wa
Chama cha Mapinduzi wa pande hizo mbili umeanzishwa kwa lengo la
kuimarisha ujirani mwema sambamba na kuimarisha Muungano wa Tanganyika
na Zanzibar wa Mwaka 1964.
Mapema
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mtoni ambae pia ni Katibu Mwenezi wa
Kata hiyo Ndugu Hija Makamba alisema Viongozi na Wanachama wa CCM wa
pande hizo mbili tayari wamekuwa na utaratibu wa kutembeleana hata
katika siku za kawaida kwa takriban miaka 20 sasa.
Ndugu
Hija alieleza kwamba ziara hizo zimekuwa zikitoa nafasi kwa wanachama na
Viongozi wa pande hizo mbili za Wilaya ya Dimani na Wilaya ya Temeke
kubadilishana mawazo ya Kisiasa na hata yale ya Kiutamaduni.
No comments:
Post a Comment