MSANII
wa kizazi kipya anayetamba na wimbo wa Chekecha Cheketua, Ali Saleh
‘Kiba’ amewapagawisha vilivyo mashabiki wake waliojitokeza katika shoo
ya Mwana Dar Live kwenye Sikukuu ya Pasaka katika Ukumbi wa Taifa wa
Burudani, Dar Live, Mbagala jijini Dar es Salaam.
Ali
Kiba akiwa sambamba na mdogo wake Abdul Kiba waliangusha bonge la
burudani huku wakiimba nyimbo zao zote kwa kutumia vyombo vya jukwaani
‘live band’.
Shoo
hiyo ilisindikizwa na Isha Mashauzi akiwa na Mashauzi Classic, Msaga
Sumu na Pamela Daffa 'Pam D' ambao walitoa burudani ya nguvu na
kuzikonga nyoyo za mashabiki waliofurika ndani ya ukumbi huo.
No comments:
Post a Comment