Awali kulikua na matukio ya kurushiana maneno katika ukumbi mkuu wa hesabu ya kura pale mwakilishi wa chama tawala-PDP Elder Orubebe alipolalamikia tume ya uchaguzi kwa kupendelea.
Kumekua na kurushiana cheche za maneno makali katika ukumbi mkuu wa kuhesabu kura nchini Nigeria.
Mwakilishi wa chama tawala PDP-Elder Orubebe, alivuruga shughuli ya kutangazwa matokeo ya kura akidai tume ya uchaguzi ilikua ikipendelea upande mmoja.
Mwenyekiti wa tume ya kitaifa ya uchaguzi mkuu Nchini Nigeria, Attahiru Jega, alimuonya Elder Orubebe kuwa mwaangalifu kutokana na matamshi yake hayo aliyotoa.
Mwandishi wa BBC aliyeko ukumbi huo mjini Abuja anasema huenda vurugu hizo ni ishara kuwa, PDP inahisi kushindwa.
Huku majimbo mengi yakitoa matokeo yake mgombea wa upinzani, Muhammadu Buhari wa chama cha APC, anaendelea kuongoza kwa wingi wa kura, huku akifuatiwa na Rais Goodluck Jonathan.
Generali Buhari wa chama cha All Progressives Congress (APC) anaonekana kusajili matokeo mema mapema hata kabla ya kuhesabiwa kwa kura za mjini Lagos.
Matokeo ya uchaguzi mkuu nchini Nigeria yanatarajiwa kutangazwa saa chache zinazokuja wakati majimbo yaliyosalia yakisubiriwa kutangaza matokeo yao.
No comments:
Post a Comment