Mwakilishi
wa Katibu Mkuu na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Mashariki ya Kati
katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw.Elibariki
Maleko(katikati) akizungumza kuukaribisha Ujumbe kutoka Chuo cha
Mafunzo ya Kijeshi cha nchini Nigeria (hawapo pichani) ulipokutana na
Watendaji wa Wizara kwa ajili ya kujifunza masuala mbalimbali yanayohusu
Sera ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa. Ujumbe huo
unaongozwa na Brigedia Generali Jimoh (wa pili kushoto) na upo nchini
kwa ziara ya mafunzo. Wengine katika picha ni Mkurugenzi wa Idara ya
Sera na Mipango, Bw.James Lugaganya ( kushoto), Kaimu Mkurugenzi wa
Idara ya Ushirikiano wa Kikanda, Bw. Innocent Shiyo (wa pili kulia) na
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Bi.Maulidah Hassan.
Mwenyeji
wa Ujumbe huo kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania, Brigedia Jenerali
Mwemnjudi (mwenye nguo nyeupe) pamoja na Mwambata wa Jeshi katika
Ubalozi wa Nigeria hapa nchini Brigedia Jenerali Erick Angaye
wakimsikiliza Bw. Maleko (hayupo pichani)
Sehemu ya Maafisa wa Jeshi kutoka Nigeria wakifuatilia kwa makini maelezo kutoka kwa Bw. Maleko |
Maofisa na Wanachuo wa Chuo cha Kijeshi cha Nigeria wakati wa mkutano huo |
Mmoja wa wanachuo akiuliza swaliwakati wa mkutano huo |
Kiongozi
wa msafara wa Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi cha nchini Nigeria, Brigedia
Jenerali Jimoh akimkabidhi zawadi ya nembo ya chuo hicho Bw. Maleko
Picha ya pamoja.
Picha na Reuben Mchome
No comments:
Post a Comment