Mkurugenzi wa mafunzo ya Yali Connect Camp, Dk. Yusuf Kalyango akizungumza na wahitimu 18 wa mafunzo hayo.
Mbunge
wa Jimbo la Arumeru Mashariki kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema),Joshua Nassary akipozi katika picha na Balozi wa Marekani
nchini Tanzania, Mark Childress mara baada ya kukabidhiwa cheti cha
uhitimu.
Na Mwandishi wetu.
Jumla
ya vijana 18 kutoka nchi za Kenya, Uganda, Mauritius, Seychelles na
Tanzania wemehitimu mafunzo ya wiki mbili ya uongozi bora yaliyoanzishwa
na Rais wa Marekani, Barrack Obama.
Mafunzo
hayo yaliendeshwa nchini chini ya programu ya Connect Camp chini ya
Mandela Washington Fellowship, Chuo Kikuu cha Ohio na Taasisi ya
Kimataifa ya Uandishi wa Habari (Institute for International Journalism)
yenye malengo ya kuwapa uwezo vijana wa kuwa viongozi bora wa baadaye.
Akizungumza
wakati wa ufungaji wa mafunzo hayo, Balozi wa Marekani nchini Tanzania
Mark Childress aliwataka vijana hao kutumia mafunzo hayo kwa mafanufaa
katika fani zao na nchi husika kwani ni nyenzo ya kuwa viongozi bora wa
baadaye hapa duniani.
Childress
alisema kuwa Rais Obama ameanzisha mafunzo hayo kutokana na kutambua
umuhimu wa uongozi bora na kuamini kuwa vijana ndiyo taifa la kesho.
“Nimefurahishwa
na mwamko wa mafunzo haya, nawaomba myatumie kwa ajili ya maendeleo
yenu na kwa nchi husika, hii ni nyenzo pekee katika kufikia lengo
mlilojiwekea,” alisema Childress.
Mafunzo
hayo yanayojuliana kwa jina la ‘Young African Leadership Initiative
(Yali) yalishirikisha vijana nane (8) wa Kitanzania, wanne Uganda, huku
Kenya, Mauritius na Seychelles zikiwakilishwa na watu wawili wawili.
Mmoja
wa wahitimu wa mafunzo hayo ni Mbunge wa Chadema jimbo la Arumeru
Mashariki, Joshua Nasari ambaye alisema atatumia mafunzo hayo
kujihimarisha kisiasa na kushinda kiti ha ubunge katika jimbo hilo.
Alisema kuwa mafunzo hayo yamepanua ufahamu wake katika siasa na hiyo ndiyo itakuwa silaha kubwa katika uchaguzi ujao.
“Najua
kuwa nitapata upinzani mkubwa katika uchaguzi huo, nipo kidete kwa
ajili ya kutetea kiti hicho na kupitia mafunzo haya, hakuna
atakayenizuia kushinda,” alisema Nasari.
No comments:
Post a Comment