PROF. ELISANTE OLE GABRIEL AFUNGUA MKUTANO WA MTANDAO WA MAWASILIANO AFRICA (ACRAN) JIJINI DAR ES SALAAM - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


29 Oct 2013

PROF. ELISANTE OLE GABRIEL AFUNGUA MKUTANO WA MTANDAO WA MAWASILIANO AFRICA (ACRAN) JIJINI DAR ES SALAAM

PIX1
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akiongea na waandishi wa habari baada ya kufungua rasmi mkutano wa Mtando wa Mamlaka za Udhibiti wa Mawasiliano Afrika (ACRAN) leo jijini Dar es Salaam.

PIX3
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (kulia) akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) Prof. John Nkoma  wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Mtandao wa Mamlaka za Udhibiti wa Mawasiliano Afrika (ACRAN) leo jijini Dar es Salaam
PIX4
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (waliokaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi wajumbe wa Mkutano wa Mtandao wa Mamlaka za Udhibiti wa Mawasiliano Afrika (ACRAN) leo jijini Dar es Salaam.
…………………………………………………………………………………………………
Na Frank Shija – WHVUM
Wadau wa sekta ya Utangazaji barani Afrika wametakiwa kulinda na kuthamini maudhui ya ndani badala ya kukumbatia madhui ya nchi za magahari.
Rai hiyo imetolea na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel alipokuwa akifungua mkutano wa Mtandao wa Mamalaka za Udhibiti wa Mawasiliano Afrika (ACRAN) leo jijini Dar es Salaam.
Profesa Elisante amesema ni faraja kubwa kuona kuwa wadau wa sekta ya udhibiti mawasiliana wanashirikiana katika kutatua na kusimamia sekta hiyo muhimu kwa pamoja kwa kuwa hiyo italeta nguvu na hari ya kusimamia maadili ya kiafrika kwa sauti moja.
“Nafarijika sana kuona mnavyo shirikiana katika kuhakikisha maudhui katika sekta ya utangazaji hayaleti athari katika maadili yetu, hivyo ni seme tu Serikali itazidi kushirikiana nanyi katika kusimamia hilo”. Alisema Prof. Elisante.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa  Mtandao wa Mamlaka za Mawasiliana Afrika (ACRAN)  Mhandishi Margaret Munyagi amesema kuwa pamoja na sekta hiyo kulazimika kuhamia katika mfumo wa Dijiti bada Mamlaka za Udhibiti wa Mawasiliano zinaendelea kuhakikisha kuwa hakuna mwanya kwa mahudhi yanayokihuka maadili.
Mwenyekiti huyo aliongeza kuwa kutoka na ushirikiano waliona wameweza kusimamia kwa karibu misindi na maudhi ya utandazaji ili kulinda maadili ya Mwaafrika.
“Tokea tuhamie mfumo wa Dijiti kumekuwa na ongezeko la masafa ya utangaziji lakini hili halijaathiri udhibiti wa maudhui kwa kuwa tumejipanga kikamilifu na tunashirikiana vizuri kuhakikisha maadili ya mwaafrika yanalindwa”. Alisema Mhandisi Munyagi.
Mkutano huu wa Mtandao wa Mamlaka za  Udhibiti wa Mawasiliano Afrika unafanyika ikiwa ni mara ya pili Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano huu, ambapo miongoni mwa mambo yatakayojadiliwa katika mkutano huo ni pamoja na namana Tanzania ilivyopiga hatua katika kuhamia mfumo wa Dijiti.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad