Na Chalila Kibuda,
Utafiti
unaonyesha kuwa magonjwa ya kifua Kikuu , Ukimwi ,Kansa pamoja na
ajali zinachangiwa na matumizi ya pombe kwa kiwango cha juu, na vijana
ndio waathirika wakubwa kutokana na kutokuwepo kwa sera ya matumizi ya
pombe.
Utafiti
huo umetolewa na Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu
–Kituo cha Mwanza (NIMR),uliofanywa katika Mikoa ya Kilimanjaro na
Mwanza na ambao ulilenga vijana kuanzia Miaka 15-24.
Wakizungumza
katika semina ya wadau wa masula ya afya leo jijini Dar es Salaam
,Watafiti wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu –Kituo
cha Mwanza (NIMR) , wamesema kuwa matumizi ya pombe nchini yako katika
kiwango cha juu na kusababisha magonjwa kuchangiwa na matumizi hayo.
Mtafiti
wa Sayansi ya Jamii wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya
Binadamu –Kituo cha Mwanza (NIMR), DK. Haika Osaki amesema katika
utafiti wa pombe zilizo kwenye mifuko (Viroba) zinanyweka kwa kiwango
cha juu na watumiaji ni vijana ambao ndio waathirika wakubwa wa magonjwa
kutokana na kutumia pombe.
Haika
amesema nchi ambazo zinafanana kiuchumi na Tanzania kama Zambia na
Malawi wamepiga marufuku uzalishaji wa pombe za Viroba kutokana na
kuona madhara ya matumizi ya pombe hiyo ambapo vijana wengi wameona ni
pombe zenye urahisi wa bei pamoja na uhifadhi wake.
Naye
Mtafiti wa NIMR Mwanza, Dk. Said Kapiga amesema kuwa wamefanya utafiti
na kuona madhara ya pombe na ongezeko la wagonjwa ambao wanatokana na
matumizi ya pombe pamoja na mabadiliko mengine ya kimaisha.
Mtafiti
wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu-Kituo cha Mwanza
(NIMR), Dk. Said Kapiga akifafanua jambo wakati akitoa mada yake ya
ufatiti wa Pombe,katika semina ya Wadau iliyofanyika jijini Dar es
Salaam.
Mtafiti
wa Sayansi ya Jamii wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya
Binadamu –Kituo cha Mwanza (NIMR) ,DK. Haika Osaki akitoa maada juu
matumizi ya Pombe za Viroba katika semina ya wadau iliyofanyika
jijini Dar es Salaam.
Mshauri
wa masuaya Afya na Familia, Dk. Ali Nzige akitoa mada katika semina ya
wadau juu madhara ya pombe,kwenye semina iliyofanyika Jijini Dar es
Salaam.
Sehemu
ya wadau wakifatilia maada za utafiti wa pombe katika mkutano
uliofanywa na Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu-Kituo
cha Mwanza (NIMR) iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mtafiti
wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu-Kituo cha Mwanza
(NIMR), Dk. Said Kapiga akizungumza ma waandishi wa habari juu ya
utafiti wa pombe nchini, wakati wa semina iliyofanyika jijini Dar es
Salaam.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Chama cha Kudhibiti Tumbaku nchini ,Dk.Lutgard Kokulinda
Kagaruki akizngumza na waandishi wa habari juu ya madhara ya Pombe
katika semina ya wadau iliyofanyika jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka)
No comments:
Post a Comment