Balozi
Tuvako Manongi Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa
akizungumza wakati wa uzinduzi wa onyesho la picha lililoandaliwa kwa
ubia baina ya Wakilishi za Kudumu za Italia na Tanzania. Onyesho hilo
linahusu huduma za afya ya mama na mtoto zinazotolewa na Taasisi isiyo
ya kiserikali ya Doctors with Africa CUAMM katika hospitali ya
Tosamaganga, Mkoani Iringa. Kushoto kwa Balozi Manongi ni Balozi wa
Italia katika Umoja wa Mataifa, Bw. Sebastioano Cardi na kulina ni mmoja
wa Wabunge kutoka Italia anayehudhuria mkutano wa 59 wa Kamisheni
kuhusu Hadhi ya Wanawake.
Balozi
Manongi akiteta jambo na Dkt. Andrea Atzori ambaye katika maelezo yake
amesema taasisi hiyo ya Doctors with Africa CUAMM inampango wa kupanua
huduma zake katika maeneo mengine ya pembezoni mwa Tanzania, mbali ya
Tosamaganga na Mikumi.
Dkt.
Andrea Atzori akiwa na Bi. Tully Mwaipopo, Afisa wa Uwakilishi wa
Tanzania katika Umoja wa Mataifa mara baada ya uzinduzi wa onyesho
hilo.
baadhi
ya picha zinazoonesha huduma ya utoaji wa afya ya mama na mtoto katika
Hospitali ya Tosamaganga , huduma hiyo ainayoendana manafumzo kwa
wataalamu wa afya imeweza kuokoa maisha ya wanawake wajawazito pamoja na
watoto wachanga wanaozaliwa kabla ya muda.
Na Mwandishi Maalum, New York
Tanzania
imeelezea kuridhishwa kwake na ushirikiano uliopo baina ya Serikali
na Taasisi Binafsi katika uboreshaji na utoaji wa huduma za afya
zikiwamo zinazomlenga mama na mtoto. Na hivyo kuchangia katika
upiguzaji wa vifo vya mama wajawazito na watoto wachanga.
Kauli
hiyo imetolewa siku ya jumatatu na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania
katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi, wakati wa uzinduzi wa
onyesho kwa njia ya picha kuhusu huduma za afya zinazotolewa na
Taasisi isiyo ya kiserikali ya Doctors with Africa CUAMM inayofanya
shughuli za utoaji wa huduma za afya ya mama na mtoto katika Hospitali
ya Tosamaganga, Mkoani Iringa.
Picha
hizo zinaonyeshwa katika corridor za Umoja wa Mataifa, sambamba na
mkutano wa 59 wa Kamisheni ya Hadhi ya Wanawake ( CSW) unaofanyika hapa
Makao makuu ya Umoja wa Mataifa, mkutano unaojadili masuala mbalimbali
yanayomhusu mwanamke na mtoto wa kike, kuanzia elimu, fursa na haki
sawa, huduma bora za afya, uwezeshwaji , haki za mwanamke na mtoto wa
kike pamoja na changamoto zinazo wakabili.
Balozi
Manongi amesema ni kwa kushirikiana ndipo nchi kama Tanzania
inaweza kuongeza kasi ya kuwafikishia huduma za afya wananchi wengi,
na kuwa uwepo wa Taasisi kama ya Doctors with Africa CUAMM na
mchango wake katika utoaji wa huduma za afya huko Tosamaganga na
maeneo mengine ni kielelezo sahihi cha ushirikiano anaouzungumzia.
Akasema
mchango wa Taasisi hiyo ni mfano wa kuigwa na ndiyo maana Tanzania
katika maandalizi ya malengo mapya ya maendeleo baada ya 2015 moja
ya maeneo inayoyapigia chapuo ni pamoja na hilo la afya ya mama na
mtoto pamoja na ushirikiano miongoni mwa wadau mbalimbali.
“
Nyinyi ni kielelezo sahihi cha ubia na ushirikiano tunaouhimiza.
Asanteni sana kwa mchango wenu na asanteni kwa kudhirisha kwamba
inawezekana kufanya kazi kwa ushirikiano”. akasema Balozi.
Kwa
upande wake Mwakilishi wa Taasisi hiyo, Bw. Andrea Atzori, amesema
Taasisi yake ambayo imekuwa nchini Tanzania tangu mwaka 1968
imejielekeza Zaidi katika utoaji wa huduma za afya katika maeneo ya
vijijini hususani kwa akina mama wajawazito na watoto wachanga
wakiwamo wanaozaliwa kabla ya muda.
Huduma
nyingine zinatolewa na taasisi hiyo ni pamoja na mafunzo kwa
wataalamu wa afya, huduma za uzazi salama kupitia mpango wao wa miaka
mitano walioupa jina la “mama na mtoto kwanza”.
Aidha
kwa mujibu wa Dkt. Andrea Atzori, Taasisi hiyo inatarajiwa kupanua
huduma zake katika maeneo mengine Zaidi ya pembezoni kwa lengo la
kuhakikisha kwamba wananchi wengi wanapata huduma ya afya pale walipo.
Pamoja
na Tanzania, Doctors with Africa CUAMM iliyoanzishwa mwaka 1950 na
makao yake yakiwa nchini Italia,pia inaendesha shughuli zake katika nchi
za Angola, Ethiopia, Msumbiji, Sudani ya Kusini, Uganda na Sierra
leone.
No comments:
Post a Comment