Mazishi : Mbunge Joshua Nassari Aongoza Mazishi ya Aliyekuwa Mwanafunzi wa IFM Emanuel P. Pallangyo, Sing'isi Meru Arusha - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Friday, 13 February 2015

Mazishi : Mbunge Joshua Nassari Aongoza Mazishi ya Aliyekuwa Mwanafunzi wa IFM Emanuel P. Pallangyo, Sing'isi Meru Arusha

Mbunge wa Arumeru Mashariki Mh. Joshua Nasary akitoa salamu za Pole kwa wafiwa wote wakati wa mazishi ya Marehemu Emmanuel Pendael Pallangyo aliyefariki Tarehe 7.02.2015 na kuzikwa kijijini kwao Sing'isi Meru tarehe 12.02.2015 .
Baba wa Marehemu Mzee Pendael T.  Pallangyo akitoa Salam zake za Mwisho kwa Mwanae Mpendwa Emmanuel Pallangyo
Kaka Mkubwa wa Marehemu Elisante Pallangyo, akifuatiwa na Dada zake Eliakunda  Pallangyo, Magreth Pallangyo pamoja na Sarah Pallangyo wakitoa Heshima za Mwisho  katika Mwili wa Marehemu Emmanuel Pendael Pallangyo Kijijini kwao Sing'isi Meru  Arusha.
Wa kwanza kulia ni Mbunge wa Arumeru Mashariki Mh.  Joshua Nasary akiwa na kwenye msiba wa Marehemu Emmanuel Pallangyo ambaye alikuwa ni Mwanafunzi wa IFM nyumbani kwao Sing'isi Meru.
Mmoja wa wanafamilia akisoma Wasifu wa Marehemu Emannuel Pendael Pallangyo
Msaidizi wa Askofu mkuu wa Jimbo la Kaskazini   Paulo Urio akiongoza Ibada ya Mazishi ya Marehemu Emmanuel Pendael Pallangyo kijijini kwao Sing'isi Meru.
Baadhi ya viongozi wa Dini kutoka Madhehebu Mbalimbali wakiwa wanaimba na waombolezaji wengine wakati wa ibada ya  Mazishi.
Mkuu wa jimbo la KKT kaskazini  Zelote Pallangyo akitoa Mahubiri wakati wa Misa ya mazishi ya Marehemu Emmanuel Pallangyo kijijini kwao Sing'isi Meru.
 Aliyeteuliwa kuzungumza kwa niaba ya Familia Bwana Exaud Assery Pallangyo akitoa salamu za shukurani za pekee kwa watu wote waliohudhuria Mazishi ya Mpendwa wao Emmanuel Pendael Pallangyo aliyefariki Tarehe 7.02.2015 Jijini Dar es salaam na kuzikwa Tarehe 12.02.2015 Nyumbani kwao Sing'isi Meru.
Baadhi ya ndugu wa Marehemu Emmanuel Pendael Pallangyo aliyefariki tarehe 7.02.2015 wakiwa na simanzi wakati wa Ibada ya Mazishi kijijini kwao Sing'isi Meru
Baadhi ya waombolezaji wakiwa katika Ibada ya Mazishi ya Marehemu Emmanuel Pallangyo kijijini kwao Sing'isi Meru.
Mwili wa Marehemu Emmanuel Pendael Pallangyo ukipelekwa Makaburini kijijini kwao Sing'isi Meru kwa ajili ya Mazishi.

No comments:

Post a Comment