Habari : Dk. Gharib Bilal Akutana na Uongozi wa Kampuni ya Mwananchi Communication - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Friday, 13 February 2015

Habari : Dk. Gharib Bilal Akutana na Uongozi wa Kampuni ya Mwananchi Communication


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mwananchi Communication, Francis Nanai,  wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Feb 13, 2015 kwa mazungumzo na kujitambulisha rasmi baada ya kuteuliwa kushika nafasi hiyo. Kushoto ni Mhariri Mtendaji wa Kampuni hiyo, Bakari Machumu.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Uongozi wa juu wa Kampuni ya Mwananchi Communication, Mkurugenzi Mtendaji Francis Nanai  (katikati) na Mhariri Mtendaji wa Kampuni hiyo, Bakari Machumu,  wakati walipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo kwa mazungumzo na kujitambulisha rasmi baada ya kuteuliwa kushika nafasi hiyo na kuelezea kazi zinazofanywa na kampuni hiyo. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Uongozi wa juu wa Kampuni ya Mwananchi Communication, Mkurugenzi Mtendaji Francis Nanai  (kulia kwa Makamu), Mhariri Mtendaji wa Kampuni hiyo, Bakari Machumu, na Mshauri wa Kampuni hiyo, Teddy Mapunda wakati walipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo kwa mazungumzo na kuelezea kazi zinazofanywa na kampuni hiyo. 
Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa juu wa Kampuni ya Mwananchi Communication, Mkurugenzi Mtendaji Francis Nanai  (wa pili kushoto) Mhariri Mtendaji Bakari Machumu (kulia) na Mshauri wa Kampuni hiyo, Teddy Mapunda (kushoto) baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam leo.

No comments:

Post a Comment