Mkuu
wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Chiku Gallawa (mwenye kilemba kichwani)
akimsikiliza Afisa Mtendaji wa Kata ya Msalato Dodoma Ndg. Herman
Malindira (kulia) akiwasilisha taarifa ya mradi wa ujenzi maabara kwenye
sekondari ya Chikole Feb. 16, 2015.
Mkuu
wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Chiku Gallawa (kushoto) akitoa maagizo kwa
viongozi wa Manispaa ya Dodoma na kata ya Msalato baada ya kutoridhishwa
na maendeleo ya ujenzi wa maabara wakati alipofanya ziara ya ukaguzi wa
Maabara Mjini Dodoma Feb. 16, 2015.
Mkuu
wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Chiku Gallawa (katikati) akionesha
kutokuridhishwa na hatua ya ujezi wa maabara kwenye sekondari ya Miyuji
inayojengwa na Kata za Miyuji na Mnadani ikiwa hatua ya msingi wakati
alipofanya ziara ya ukaguzi wa Maabara Mjini Dodoma Feb. 16, 2015,
Amemuagiza Mkurugenzi Manispaa ya Dodoma kuwachukulia hatua watendaji
wote walioshindwa kusimamia ujenzi wa maabara.
Mkuu
wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Chiku Gallawa (katikati) akiwaagiza viongozi wa
Manispaa ya Dodoma na kata ya Chamwino kufanya kazi kwa kushirikiana na
wananchi na wadau mbalimbali kuhakikisha wanakamilisha ujenzi wa maabara
sekondari ya Chinangali ifikapo mwishoni mwa mwezi Aprili, Mhe. Gallawa
ameonesha kutokuridhika na ujenzi wakati alipofanya ziara ya ukaguzi wa
Maabara Mjini Dodoma Feb. 16, 2015 na kukuta maabara ik kwenye hatua ya
ujenzi wa msingi.
Mkuu
wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Chiku Gallawa (kushoto) akiwaagiza viongozi wa
Manispaa ya Dodoma na kata ya Chang’ombe kuhakikisha wanakamilisha
ujenzi wa maabara sekondari ya Lukundo ifikapo mwishoni mwa mwezi
Aprili, Mhe. Gallawa ameonesha kutokuridhika na ujenzi wa Maabara
Manispaa ya Dodoma wakati alipofanya ziara ya ukaguzi wa Maabara Feb.
16, 2015.
No comments:
Post a Comment