Na Annastazia Rugaba, PDB habari
Mtendaji
mkuu wa Ofisi ya Rais, usimamizi wa utekelezaji wa miradi (PDB) Bwana
Omari Issa, leo amekabidhi rasmi taarifa ya mkakati wa kuboresha sekta
ya afya chini ya BRN kwa jumuia ya wahisani wa maendeleo.
Makabidhiano
hayo yamefanyika katika ofisi za PDB ambapo jumuiya ya wahisani ilipata
fursa ya kusikiliza kwa kina namna BRN inavyofanya kazi ya kuleta
matumaini mapya kwa watanzania kupitia sekta za kipaumbele.
Sekta ya afya imekuwa ikijaribu kuboresha utendaji wake lakini kuingia
katika BRN kutaleta tija Zaidi.
BRN
inaamini katika misingi mikuu ambayo ni kuweka vipaumbele, kuwa na adabu
ya utekelezaji, uwajibikaji na uaminifu, ufuatiliaji wa kina na wa mara
kwa mara na Mawasiliano thabiti kati ya watoa huduma na wapokea
huduma.
Hizi
ni nguzo muhimu zitakazotufikisha katika dira ya maendeleo ya taifa ya
Mwaka 2025.
Awamu ya kwanza ya BRN iliziangazia sekta sita ambazo ni Kilimo, Elimu,
Maji, Uchukuzi, Nishati na ukusanyaji wa mapato ambapo sekta za Afya na
Uboreshaji wa mazingira ya Biashara zimeanza rasmi Mwaka huu.
Sekta
sita za mwanzo zimedhihirisha mafanikio anuwai ambayo yaliwavutia jopo
la wataalamu wa maendeleo wakiongozwa na Rais Mstaafu wa Botswana Bw
Mogae. Ripoti kamili ya utekelezaji wa BRN kwa Mwaka wa kwanza
itazinduliwa rasmi mapema mwezi Machi Mwaka huu.
Sekta
ya afya inakusudia kutekeleza vipaumbele vine ambavyo ni mosi;
ugawanyaji sawia wa wahudumu wa afya wenye ujuzi takikana kuanzia ngazi
ya chini ya afya ya msingi, pili; utoaji huduma wenye ubora wa nyota
tatu katika ngazi zote, tatu; upatikanaji wa dawa na bidhaa muhimu za
afya katika ngazi zote, nne; kuimarisha afya ya uzazi na usalama wa mama
na mtoto ili kupunguza vifo vya kundi hili muhimu kwa angalau asilimia
60 ifikapo Mwaka 2018.
Jumuiya
ya wahisani wamepongeza uamuzi wa kuiingiza sekta ya afya katika BRN na
wakithibisha utayari wao wa kufanikisha mkakati huu, wametoa wito kwa
wizara ya afya, PDB, Sekta binafsi na jamii ya kitanzania kwa ujumla
kuhakikisha kuwa mkakati huu utafanikiwa.
Malengo
haya yote yanahitaji juhudi kubwa na ya pamoja kutoka kwa jamii, wizara
na taasisi zake zote hadi ngazi ya kijiji, wahisani wa maendeleo na
sekta binafsi.
“Tusingoje
nani aanze, sote tuwajibike, kila mmoja ajitazame kama anawajibika
ipasavyo. Dira ya maendeleo ya Taifa tunayotaka itupeleke kuwa nchi
yenye uchumi wa kati haiwezi kufikiwa tusipofanya kazi kwa pamoja bila
kunyoosheana vidole.
BRN ni
treni iliyoanza safari tayari, kila mmoja anawajibika kuingia kwa
wakati na kwa nia Chanya, ukichelewa ukakuta imeondoka bado una fursa ya
kuikimbilia kituo kinachofuata ili twende pamoja” Bw Omari Issa ametoa
wito huo kwa wahisani wa maendeleo na jamii kwa ujumla.
Mtendaji
Mkuu wa PDB Bw. Omari Issa akielezea umuhimu wa sekta ya Afya kuingia
BRN kuungana na sekta nyingine zilizotangulia zinazoendelea kuzaa
matunda
Dr
Linda Ezekiel ambae ni Mkurugenzi wa sekta za jamii (Afya, Elimu na
Maji) PDB akiwasilisha mada kuhusu malengo ya kipaumbele sekta ya afya
kwa miaka
Bw. Omari Issa akimkabidhi mwakilishi wa wahisani wa maendeleo mkakati wa sekta ya Afya chini ya BRN
Bw Issa na Dr. Sudha Sharma wa UNICEF Tanzania ambae anawawakilisha jumuiya ya wahisani wa maendeleo baada ya makabidhiano
Mwakilishi wa jumuiya ya wahisani akipongeza uamuzi wa serikari kuiweka sekta ya afya katika BRN
Naibu
Katibu mkuu wa wizara ya afya Bw Michael akiwashukuru PDB kwa kusimamia
vizuri mchakato wa kuchagua vipaumbele vya sekta ya afya chini ya BRN
Mmoja wa wahisani akisisitiza suala la uwajibikaji katika sekta ya af
Bi. Sharon Crommer Mkuu wa USAID Tanzania akisisitiza ushiriki wa sekta Binafsi katik kuboresha Sekta ya afya Nchini Tanzania
Mmoja wa wahisani akisisitiza umuhimu wa wizara ya afya kuwajibika ki BRN katika maeneo mengine yasiyo ya kipaumbele katika BRN
Dr
Oberline Kisanga wa kitengo cha mageuzi katika wizara ya afya
akifafanua ushiriki wa TAMISEMI katika mkakati huu wa afya chini ya BRN
Bw Mugisha na Dr Linda wa PDB wakifurahia sehemu ya makabidhiano ya mkakati wa afya chini ya BRN
Sehemu ya washiriki wa tukio hili wakiwa katika ukumbi wa mkutano wa PDB
No comments:
Post a Comment