Na Rashda Swedi- OMR
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira Mhe. Dkt. Injinia Binilith
Mahenge amepiga marufuku matumizi ya magogo kama nishati ya kuzalisha
bidhaa katika viwanda.
"Matumizi
ya Magogo viwandani kama nishati ya uzalishaji ni uharibifu mkubwa wa
Mazingira na ni adui wa maendeleo katika Taifa letu, pia ni teknolojia
iliyopitwa na wakati".
Hayo
yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira Mhe.
Dkt. Injinia Binilith Mahenge alipotembelea kiwanda cha kutengeneza Nguo
cha Afirtex kilichopo Jijini Tanga. Alisema hayo baada ya kukuta
kiwanda hicho kinatumia magogo kama nishati ya uzalishaji.
Hata
hivyo ameutaka uongozi wa kiwanda hicho kuhakikisha hatatumia tena
magogo na badala yake watumie nishati mbadala kwa mfano makaa ya Mawe
ili kuweza kulinda Mazingira.
Alisisitiza
kwa kusema kuwa Matumizi ya Magogo katika uzalishaji ni Teknolojia ya
zamani hivyo tunatakiwa tubadilike ili kukabiliana na Mabadiliko ya
Tabianchi ambayo kwa sasa ni pigo kubwa kwa Taifa letu kutokana na
ukataji miti hovyo.
Aidha,
amewapa miezi mitatu kuwacha kabisa kutumia magogo katika uzalishaji na
endapo wakibainika wanaendelea kutumia magogo hatua za kisheria
zitachukuliwa.
Hata
hivyo, Mhe. Mahenge aliutaka uongozi wa kiwanda hicho kuchimba bwawa
litakalotumika kwa ajili ya kuondoa sumu zilizokuwa kwenye maji
yanayotoka kiwandani kabla ya kutiririsha katika mfereji mkuu wa maji
na kuathiri wananchi.
Wakati
huo huo Mhe. Mahenge alitembelea kiwanda cha chokaa cha Neelkanth
pamoja na kiwanda cha vipodozi LPPT kukagua hali ya Mazingira katika
viwanda hivyo.
Mhe.Mahenge
amekipongeza kiwanda cha kutengeneza vipodozi (LPPT) kwa kushiriki
usafi kila jumamosi ya mwanzo wa Mwezi ikiwa ni moja ya agizo
lililotolewa na Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe.Dkt Mohammed Gharib Bilal.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira Mhe. Dkt. Injinia Binilith
Mahenge, akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Tanga pamoja na
Wadau wa Mazingira na Waandishi wa Habari kuhusu umuhimu wa kutunza
Mazingira na athari mbalimbali zitokanazo na uharibifu wa Mazingira,
alipowasili Jijini Tanga kabla ya kuanza ziara yake.
Sehemu
ya wadau mbalimbali wa Mazingira wakisikiliza kwa makini Hotuba ya Mhe.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira Dkt. Injinia
Binilith Mahenge (hayupo pichani).
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira Mhe. Dkt. Injinia Binilith
Mahenge (aliyenyanyua mkono,) akitoa maelekezo kwa injinia wa kiwanda
cha Afritex Bw. Joseph Mhando (wa tatu kushoto) ,kuhusu kutotumia magogo
kama nishati ya uzarishaji, alipotembelea kiwanda hicho Jijini Tanga.
Injinia
wa kiwanda cha Afritex Bw. Joseph Mhando (wa kwanza kulia), akitoa
maelezo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira Mhe. Dkt.
Injinia Binilith Mahenge (wa pili kulia), jinsi wanavyoyatibu majitaka
yanayotoka kiwandani hapo kabla ya kutiririsha kwenye mfereji mkuu.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira Mhe. Dkt. Injinia Binilith
Mahenge (kulia),akikagua Mazingira ya kiwanda cha chokaa (Neelkanth
Lime) kilichopo Jijini Tanga. pembeni yake ni Mkurugenzi wa Kiwanda
hicho Bw. Rashid A. Mahmoud.
Mwenyekiti
wa kiwanda cha kutengeneza Vipodozi Bw. Mohammed Raza Hassanali (wa
tatu kulia) akitoa maelezo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais -
Mazingira Mhe. Dkt. Injinia Binilith Mahenge (wa pili kushoto), jinsi
wanavyoyasafisha maji taka kabla ya kutiririsha kwenye mfereji mkubwa.
No comments:
Post a Comment