Mwenyekiti
wa Bodi wa Busara Promotions, wandaaji wa tamasha la Sauti za Busara,
Simai Mohammed (katikati) akiongea na wandishi wa habari (Hawapo
pichani) wakati wa mkutano wa wanahabari Jijini Dar es Salaam, juu ya
tamasha la 12 la Sauti za Busara, litakalofanyika, Februari 12 hadi 15,
mwaka huu, Ngome Kongwe, Zanzibar. Wengine (kushoto) ni Meneja wa
tamasha hilo, Journey Ramadhani. na upande wa kulia ni Mkurugenzi wa
tamasha hilo, Yusuf Mahmoud 'Dj Yusuf, akifuatiwa na msanii wa bongo
fleva nchini, Ali Kiba (kulia).
Ali
Kiba katika pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Busara Promotions, Simai
Mohammed, muda mfupi baada ya utambulisho wa msanii huyo juu ya kupiga
shoo kwenye tamasha la 12 la Sauti za Busara, litakalofanyika Februari
12 hadi 15, Zanzibar.
Simai,
Dj Yusuf na Kiba wakiwa wameunganisha mikono kwa kusalimiana ikiwa ni
ishara ya Umoja na Amani, kama Kauli mbiu ya mwaka huu ya tamasha hilo
inavyohimiza amani.
Mkali
wa muziki wa kizazi kipya nchini, Ali Kiba ametamba kukonga nyoyo watu
mbalimbali watakaojitokeza kwenye tamasha la 12 la Sauti za Busara
linalotarajia kufanyika, Februari 12 hadi 15, Ngome Kongwe, Zanzubar.
Ali
Kiba alieleza hayo leo Alhamisi, Januari 29. wakati wa mkutano wa
ulioandaliwa na Busara Promotions, wandaaji wa tamasha hilo kubwa la
Kimataifa linalofanya muziki wa 'Live', ambapo kwa mwaka huu zaidi ya
wanamuziki na vikundi 37, watatoa burudani kwenye tamasha hilo kwenye
viunga vya Ngome Kongwe, Unguja, Zanzibar.
Akizungumza
mbele ya wandishi wa habari, Ali Kiba alisema kwa sasa amejiandaa kutoa
burudani ya aina na ambayo itakonga nyoyo kwa watu wote watakaojitokeza
kushuhudia tamasha hilo.
"Hii
itakuwa ni zawadi kwa watanzania wote kunishuhudia nikiimba 'live' bila
kutumia 'cd' kama wafanyavyo wengine. Mimi ni mwanamuziki na nimesoma
muziki hivyo nitapiga muziki wa nguvu jukwaani" alisema Ali Kiba.
Na
kuongeza kuwa, kwa sasa yupo kwenye mazoezi ya muda mrefu wa kujifua na
bendi maalum kwa ajili ya shoo hiyo huku akitamba kuwa, yeye ni msanii
kwani muziki aliusomea na kujifunza huko nyuma alipokuwa katika Nyumba
ya kuibua vipaji THT, ambapo alijifunza vitu vingi ikiwemo kuimba muziki
wa bendi na 'live'.
Aidha, aliwaomba wapenzi na wadau wa muziki kujitokeza kwa wingi
kushuhudia tamasha hilo kwani wasanii mbalimbali wa ndani na nje watatoa burudani ya kipekee.
Kwa
upande wake, Mwenyekiti wa bodi ya Busara Promotion, wandaaji wa tamasha
hilo, Simai Mohammed, alisema tamasha limeweza kuongeza ajira na uchumi
wa Zanzibar kwani pia limeongeza fursa za utalii.
Kwa
upande wake, Meneja wa tamasha hilo, Journey Ramadhani, alisema tamasha
hilo limeweza kuongeza fursa kila mwaka ikiwemo kutoa ajira kwa vijana
wa kitanzania kwa asilimia 90, ambapo kwa mwaka huu wanatarajia kuwa na
watendaji kazi na wa kujitolewa watakolipwa katika kusaidia tamasha
hilo, zaidi ya watu 150.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa tamasha hilo, Yusuf Mahmoud 'Dj Yusuf'
alisema tamasha hilo limeweza kuibua wasanii mbalimbali ikiwemo
kujitangaza kimataifa.
Aidha,
Dj Yusuf alieleza kuwa, tamasha la mwaka huu litaendana na kauli mbiu
ya kuimiza Amani, pia wameandaa tuzo maalum na zawadi maalum kwa wasanii
wa Tanzania watakaoshinda katika kutunga nyimbo za amani.
Mbali
na Ali Kiba, Wasanii wengine Isabel Novella kutoka Msumbiji, Ihhashi
Elimhlophe (Afrika Kusini), Tcheka (Cape Verde), Diabel Cissokho
(Senegal), Culture Musical Club (Zanzibar), Msafiri Zawose (Tanzania),
Aline Frazão (Angola), Tsiliva (Madagascar), Leo Mkanyia and the
Swahili Blues Band (Tanzania), Mohamed Ilyas & Nyota Zameremeta
(Zanzibar), Thaïs Diarra (Senegal / Mali / Uswisi), Liza Kamikazi
and band (Rwanda), Erik Aliana (Cameroon), Mpamanga (Madagascar),
Mgodro Group (Zanzibar), Rico Single & Swahili Vibes (Zanzibar),
Zee Town Sojaz (Zanzibar), Ifa Band (Tanzania) na wengine wengi.
Maelezo zaidi yanapatikana katika www.busaramusic.org
No comments:
Post a Comment