Matokeo ya Kidato cha Pili : Baraza la Mitihani la Tanzania Latangaza matokeo ya Kidato cha Pili 2014 - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


19 Jan 2015

Matokeo ya Kidato cha Pili : Baraza la Mitihani la Tanzania Latangaza matokeo ya Kidato cha Pili 2014

KWA MATOKEO YA KIDATO CHA PILI, BOFYA HAPA KWA URAHISI

Pichani niKatibu Mkuu wa Baraza la Mitiani nchini NECTA Dkt Charles E Msonde Akizungumza leo na Waandishi wa Habari jijini Dar Es Salaam 
NA KAROLI VINSENT
BARAZA la Mitihani nchini NECTA limetangaza matokea ya kidato cha pili yaliyofanyika mwaka jana 2014 huku idadi kubwa ya wanafunzi wakiwa wamefaulu na kujiunga kidato cha tatu, ikiongeza kwa asilimia 92.66 ikilinganisha na mwaka 2013 ambapo idadi ya wanafunzi waliofaulu ilikuwa asilimia 89.34.
Matokeo hayo yametangazwa leo Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Baraza la Mitihani nchini NECTA Dkt Charles E Msonde wakati wa mkutano na waandishi wa Habari ambapo alisema watahiniwa waliofanya mtihani huo uliofanyika mwezi Novemba mwaka jana ilikuwa 405,204 sawa na asilimia 89.40 Kati ya hao wasichana walikuwa 233,834 sawa na asilimia 51.60 na wavulana walikuwa 219,357 sawa na asilimia 48.40.
Dkt Msonde alisema kati ya watahiniwa hao waliofaulu na kupata alama na kuweza kuendelea na kidato cha tatu walikuwa 375,434 Sawa na asilimia 92.6 ya watahiwa wote waliofanya mtihani huo ambapo wasichana walikuwa 195,328 sawa na asilimia 92.8 na wavulana 180106 sawa na aslimia 92.69.
Aidha,Dokt Msonde aliwataja watahiniwa ambao wamepata alama ambazo hawawezi kuendelea na kidato cha Tatu na itawanalazimu kurudia kidato cha pili walikuwa 29770 kati ya asilimia 7.34.
Vilevile ,Dokta Msonde aliyetaja masomo waliofanya vizuri wanatahiniwa hao ni ya Uraia,Historiya,Kiswahili,kingereza,jeografia
Waandishi wa Habari wakimsikiliza kwa Makini 
Pia Masomo waliofanya vibaya watahiniwa hao ni ya Hesabu,Kemia,kilimo,Somo la Biashara pamoja na Biolojia.
Alibanisha kuwa sababu iliofanya idadi ya wanafunzi mwaka huu kuwa mazuri imetokana na mipango mizuri ya serikali huku ikizingatia sasa kuwepo na mfumo mpya wa matokea mkubwa sasa na akawata walimu na wazazi waendeleea kutoa mshikamano kwa walimu.
Matokeo yote ya Kidato cha pili yatakuwepo kwenye Mtandao wa baraza la Mitiani nchini,tovuti ya Wizara ya Elimu na Ofisi ya Wazari Mkuu Tamisemi, pamoja na Kwenye shule husika ya Mwanafunzi anayesoma.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad