Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati, Maji na Mafuta (Ewura), Felix
Ngamlagosi (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari
ofisini kwake Dar es Salaam leo, kuhusu mwenendo wa bei za mafuta nchini
na katika soko la Dunia. Kulia ni Mkurugenzi wa Petroli, Godwin Samwel.
Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.
Na Dotto Mwaibale,Habari za Jamii Blog
MAMLAKA
ya Udhibiti wa Nishati, Maji na Mafuta (Ewura), imepunguza bei za
mafuta kote nchini kuanzia leo kutokana na kudorora kwa uchumi wa bara
la ulaya.
Hayo
yalibainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati,
Maji na Mafuta (Ewura), Felix Ngamlagosi wakati akizungumza na waandishi
wa habari ofisini kwake Dar es Salaam leo mchana, kuhusu mwenendo wa
bei za mafuta nchini na katika soko la Dunia.
Alisema
kuanzia leo bei ya mafuta ya petroli kwa lita moja itauzwa sh.1955 na
hiyo inatokana na kushuka kwa jumla ya asilimia 16 sawa na pungufu kwa
jumla ya sh.311 kwa lita.
Alisema
bei ya petroli katika soko la dunia imeshuka kwa jumla ya aasilimia 25
kuanzia Julai hadi Novemba 2014, sawa na pungufu kwa jumla ya dila 249
kwa tani.
Ngamlagosi
alisema mafuta ya dizeli kwa lita moja yatauzwa sh.1846 na kuwa bei
hiyo imeshuka kwa asilimia 13 sawa na pungufu kwa jumla ya sh.244 kwa
lita na kuwa dizeli kwa soko la dunia imeshuka kwa jumla ya asilimia 28
kuanzia Julai hadi Novemba 2014 sawa na pungufu kwa jumla ya dola 189
kwa tani na kuwa mafuta ya taa yatauzwa sh. sh.1833 kwa lita.
Alisema
katika kipindi cha robo ya mwisho wa mwaka kuanzia mwezi Septemba hadi
Desemba 2014, bei za mafuta ghafi zimekuwa zikishuka kwa kasi
ikilinganishwa na kipindi cha hapo nyuma ambapo zimeshuka toka dola 100
kwa pipa hadi kufikia wastani wa dola 60 kwa pipa moja ambayo ni sawa na
karibu asilimia 40.
Alisema
viwango hivyo vya bei iliyopungua ni katika soko la Dar es Salaam na
mikoa mingine bei zao zimepangwa kutokana na kuwepo kwa gharama za
usafirishaji.
Ngamlagosi
alitoa mwito kwa wanunuaji wa mafuta hayo kuhakikisha wanapatiwa lisiti
baada ya kununua kwani itasaidia kuwabaini wafanyabiashara wasio
waaminifu ambao wataendelea kuuza kwa bei ya zamani.
"Natioa
mwito wa kuwaomba wanunuaji wa mafuta kuhakikisha wanapewa lisiti kwani
itatusaidia kuwabaini wale wanauza kwa bei ya juu, na pia itamsaidia
mnunuzi iwapo atauziwa mafuta yaliyochini ya kiwango na ukusanyaji wa
kodi ya serikali" alisema Ngamlagosi.
Naye
Mkurugenzi wa Petroli, Edwin Samwel alisema Ewura imejipanga vizuri
kuhakikishha hakuna ujanja ujanja utakaojitokeza wa kudai mafuta
yamekwisha au yaliyopo yatauzwa kwa bei yaliyonunuliwa.
Alisema
mfanyabiashara yeyote atakayekiuka utaratibu huo atachukuliwa sheria
pamoja na kufungiwa biashara yake ingawa alisema hali hiyo
haitajitokeza.
No comments:
Post a Comment