Na Editha Karlo ,Kigoma
KAMANDA
wa Kikosi cha Jeshi la kujenga Taifa (JKT) 824 KJ cha Kanemwa wilaya ya
Kakonko Mkoani Kigoma Luteni Kanali Erasmus Bwegoge ameomba Halmashauri
ya wilaya hiyo kutilia mkazo na kuhitimisha mchakato wa kupata hati
miliki ya maeneo ya kikosi hicho ili kuondoa uwezekano wa wananchi
kuvamia maeneo hayo jambo ambalo linaweza kuzua migogoro na kuhatarisha
mahusiao baina ya Jeshi na wananchi.
Luteni
kanali Bwegoge ametoa ombi kwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Luteni kanali
mstaafu Issa Machibya wakati wa mahafali ya nne ya kuhitimu mafunzo ya
jeshi kwa mujibu wa sheria .
''Mgeni
rasmi tunaomba Halmashauri yetu ya Kakonko suala la kupata hati miliki
ya maeneo ya kikosi chetu hiki,hii itatusaidia sana kuondoa migogoro ya
ardhi baina ya wananchi na jeshi,pia itasadia kutokuwepo na wananchi
wanaovamia katika maeneo ya jeshi''alisema.
Alisema
kuwa pamoja na kuwepo kwa changamoo hiyo ya ardhi kikosini hapo pia
kuna changamoto za huduma bora za afya alisema jumla ya vijana 1127 wa
oparesheni ya miaka 50 ya muungano wamehitimu mafunzo hayo ambao ni
wahitimu wa kozi ya ualimu na wale waliomaliza kidato cha sita
.
Kwa
upande wake mwakilishi wa mkuu wa Jeshi la kujenga Taifa nchini(JKT)
Meja Abdulrahmani Dachi na mgeni rasmi katika maafali hayo Mkuu wa M koa
wa Kigoma Luten Kanali mstaafu Issa Machibya wamewataka vijana hao
kutumia mbinu walizojifunza kudumisha ulinzi na usalama wa nchi pamoja
na kuhamasisha shughuli za maendeleo katika jamii na si kulihujumu Taifa
kwa namna yeyote.
''Muende
mkawe mfano wa kuigwa katika jamii pia mtumie mbinu mlizofundishwa
katika kudumisha ulinzi na usalama wa nchini pia mkawe mfano katika
shughuli za maendeleo katika jamii''alisema Mkuu wa Mkoa
Baadhi ya wahitimu wa mafunzo ya Jeshi la kujenga Taifa katika kikosi cha 824 KJ Kanembwa wakiwa tayari kwaajili ya Gwaride.
Wahitimu wakipita mbele ya mgeni (hayupo pichani)Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kanali mstaafu Issa Machibya rasmi kwa mwendo wa pole.
Mkuu
wa Mkoa wa Kigoma Kanali Mstaafu Issa Machibya akiwa amesimama kwa
ukakamavu wimbo wa Taifa ukiimbwa kwaajili ya ufunguzi wa sherehe za
maafali ya kufunga mafunzo ya JKT katika kikosi cha 824KJ Kanembwa.
Baadhi ya wahitimu wa mafunzo ya JKT kikosi cha 824 KJ wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi katika maafali yao ya kufunga mafunzo.
(picha zote na Editha Karlo)
No comments:
Post a Comment