Mwezeshaji kutoka
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Ester Riwa wa pili kulia akizungumza
na Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya ya Kyela Dr. Festo Dugange jana wakati wa ziara
ya kuhamasisha vijana wa Kyela. Wa kwanza kulia ni Afisa Maendeleo ya Vijana
Bi. Amina Sanga, wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Kituo cha Vijana Sasanda Mbeya
Bw. Laurean Masele na wa pili kushoto ni Afisa Vijana Mkoa wa Mbeya Bw. George
Mbijima.
Afisa
Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Amina Sanga
akiwaelimisha vijana wa Wilaya ya Kyela kuhusu mwongozo unaosimamia Mfuko wa
Maendeleo ya Vijana wakati wa semina ya Ujasiriamali, Stadi za Maisha, Ujuzi na
Mfuko wa Maendeleo ya Vijana iliyofanyika jana katika Wilaya ya Kyela Mkoa wa
Mbeya.
Vijana
wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela Mkoa wa Mbeya walioudhuria semina ya
Ujasiriamali, Stadi za Maisha, Ujuzi na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana wakifuatilia
mambo mbalimbali yaliyokua yakiendelea wakati wa semina hiyo.
Vijana
wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela wakiwa katika kikundi kujadiliana namna ya
kuandika andiko la mradi baada ya kupata mafunzo ya jinsi ya kuandika andiko la
mradi wakati wa semina ya Ujasiriamali, Stadi za Maisha, Ujuzi na Mfuko wa
Maendeleo ya Vijana iliyofanyika jana katika Wilaya ya Kyela Mkoa wa Mbeya.
Mwenyekiti
wa Wadau Self Supporting Group Bw. Godbless Konga wanne kulia akizungumza na
maafisa kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo walipotembelea
kikundi hicho kuangalia mradi unaoendeshwa na vijana wa kikundi hicho jana
wakati wa ziara ya kukagua miradi ya vijana wa Wilaya ya Kyela Mkoa wa Mbeya.
No comments:
Post a Comment