Timu
ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango
wakiwasili kwenye Bandari ya Bukoba, walipofika kujionea bandari hiyo
kongwe iliyopo kwenye fukwe za Ziwa Victoria, mkoani Kagera.
Waliotangulia mbele ni Kiongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya
Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri
(Wapili kulia). Wengine ni baadhi ya wajumbe wa msafara huo kutoka
kushoto ni Bw. Omary Abdallah, Bibi Zena Hussein (Wapili kushoto) na Bw.
Julius Edward (Kulia).
Madhari ya gati la Bandari ya Bukoba.
Wajumbe
wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya
Mipango wakiwa kwenye ngazi za kupandia kwenye meli zinazotia nanga
kwenye Bandari ya Bukoba.
Wajumbe
wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya
Mipango wakiwa kwenye Ofisi za Bandari ya Bukoba. Jengo la Ofisi hiyo
limejengwa takriban miaka 70 iliyopita.
Sehemu ya kupumzikia abiria ya Bandari ya Bukoba.
Wajumbe
wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya
Mipango wakiwa kwenye moja ya maghala ya kuhifadhia mizigo kwenye
Bandari ya Bukoba. PICHA NA SAIDI MKABAKULI
No comments:
Post a Comment