Mvua na Maafa : Taswira ya Mvua Kubwa iliyonyesha Jana Jijini Dar es Salaam - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


30 Dec 2014

Mvua na Maafa : Taswira ya Mvua Kubwa iliyonyesha Jana Jijini Dar es Salaam


 Baada ya mvua ya kama vigudulia kadhaa hili iliyomwagika kwa masaa mawili mfululizo,maeneo mengi jijini Dar yameungana na bahari ya hindi kwa kujaa maji na kupelekea adha kubwa kwa wakazi wa jiji hili.Pichani ni eneo la barabara ya Morogoro Road.
 Matolori ya kuuzia ice creame yakionekana kununiwa leo,huku wapita njia wakiendelea kupiga mbizi kwenye maji hayo.
 Barabara ya Bibi Titi Mohamed mambo yalikuwa namna hii,wenye magari madogo walipita kwa staili ya maji ya shingo.
 Hapa tena,mwendo wa viatu mkononi.
 Kipando nacho kimeroga.
 Hapa ndio inakuwaga kimbebe,maana daladala ndio lishabuma tena.
 "Hii mvua isharoga tena,na huu mwamvuli miyeyusho kweli".
 mvua ikiendelea kupiga.
 Huu mtaa wa naniii....
Hapa dawa ni kutoka nduki tuu...
Kipini cha nguvu barabara ya Umoja wa Mataifa kutokea Faya.


Hakuna namna nyingine ya kuyakwepa maji haya.hapa ni Posta mpya jana.

Posta mpya mambo inogilee.
Mojaaa..... mbiliii.... taaaatuuuuu...... Shtuaaaaa..
Jamaa wakipiga kibeda Nadia iliyobuma katikati ya barabara,maeneo ya Sinza.
Hapa ni Bamaga Jana.Picha na Othman Michuzi wa Mtaa kwa Mtaa Blog

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad