Mfuko wa Jamii : PSPF Yatoa zawadi za Krismasi kwa Kituo cha Kulelea Watoto Yatima cha Amani Orphanage Center, Pwani - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Saturday, 6 December 2014

Mfuko wa Jamii : PSPF Yatoa zawadi za Krismasi kwa Kituo cha Kulelea Watoto Yatima cha Amani Orphanage Center, Pwani

Kushoto ni Meneja wa Pwani wa PSPF Msafiri S. Mugaka  akiwa na Afisa Mahusiano wa PSPF Coleta Mnyamani wakiwakabidhi zawadi ya Mbuzi  kwa ajilli ya Krismasi watoto wa kituo cha kulelea yatima cha Amani Orphanage Centre tarehe 5.12.2014
 Afisa Mahusiano wa PSPF Coleta Mnyamani akimkabidhi zawadi ya vinywaji mmoja wa watoto katika kituo hicho
 Meneja wa Pwani wa PSPF Msafiri S. Mugaka akimkabidhi mmoja wa watoto msaada wa mafuta ya kupikia kwa niaba ya watoto wenzake walipo watembelea katika kituo chao huko  Zinga Bagamoyo
 Kati kati ni Mwanzilishi wa Kituo hicho cha watoto yatima na Mkurugenzi mkuu wa Kituo hicho Bi. Magreth Mwegalawa akikabidhiwa zawadi ya unga kwa ajili ya kituo cha watoto hao yatima na Mfuko wa Pensheni wa PSPF
Watoto , Walezi, pamoja na ma Afisa wa PSPF wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukabidhi zawadi kwa watoto kwa ajili ya Sikukuu ya Krismas
Kutoka Kulia  ni Afisa wa PSPF Mhina, Afisa Ustawi wa Jamii Bagamoyo Flora Walioba ,Afisa Mahusiano wa PSPF Coleta Mnyamani, Meneja wa Mfuko wa PSPF Pwani Msafiri S. Mugaka na Afisa Ustawi wa Jamii wa Bagamoyo Rajabu Mturuya 
Watoto wa Kituo cha Amani Orphanage Centre Wakiimba wimbo wa Taifa wakati wanawakaribisha wageni kutoka Mfuko wa Pensheni wa Pspf 
Meneja wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF Mkoa wa Pwani Msafiri Mugaka akizungumza na watoto katika kituo cha Kulelea watoto yatima cha Amani Orphanage Centre kilichopo Zinga Bagamoyo, Alisema kuwa Mfuko wa Pemsheni wa PSPF umeguswa sana na vituo mbalimbali vya kuwalea watoto yatima kikiwemo na cha Amani Orphanage Centre ambapo pamoja na kuwapelekea zawadi za Sikukuu ya Krismas , lakini kutokana na Kituo hicho watoto kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu watasoma watakuwa wakubwa na wakianza kazi nao watajiunga na PSPF kwa kuwa hata mtu binafsi kama anakipato tuu anaweza kujiunga na Mfuko huo. 
Afisa Mahusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF Coleta Mnyamani akiongea na watoto pamoja na walezi wa Kituo cha Amani Orphanage Centre ambapo alisisitiza kuwa watoto wasijisikie vibaya kwa kuwa wengine hawana wazazi au wamekuja katika kituo hicho kwa matatizo mbalimbali na kwamba PSPF wameguswa na ndio maana wamewatembelea kuwaona pia kuwaletea msaada na zawadi mbalimbali ili nao waone kuwa wapo katika jamii moja kuwa hakuna tofauti kati ya watoto yatima na wenye wazazi.
Afisa Ustawi wa Jamii wa Bagamoyo Rajabu Mturuya   akiwakaribisha ma Afisa wa PSPF katika kituo hicho cha kulelea watoto yatima 
 Mkurugenzi wa Kituo cha Kulelea watoto yatima Cha Amani Orphanage Centre  Magreth Mwegalawa akisoma hotuba kwa wageni ambapo aliwashukuru kwa kuja kuwaona pia alisema kituo hicho kimesajiliwa kwa namba 000NGO/3288 na kimeanzishwa mwaka 2008 ambapo kuna jumla ya watoto 50 wakiume 19 na wakike 31.
Mlezi wa watoto wa Kituo cha Amani Orphanage Centre Bibi Titi 
Mtoto Haji Akitoa neno la Shukurani kwa Mfuko wa Penshemi wa PSPF kwa zawadi walizopewa na mfuko huo.
Watoto wakiwasikiliza kwa makini ma Afisa wa PSPF ambao hawapo pichani
Afisa Mahusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF Coleta Mnyamani  akiwa anatoa zawadi kwa watoto
Julia Richard akiwa na Mtoto Getruda Shabani aliyechukuliwa na Kituo hicho akiwa na umri wa siku nne na mpaka sasa anasiku 40 mtoto huyu hana wazazi.
 Watoto wakipata Burudani 
Wakati Mwezi wa Kumi na Mbili Ukiwa Unaendelea Kuyoyoma Nayo Maandalizi ya Kusherehekea Sikukuu ya Kuzaliwa Kwa Mokozi yakiwa Yamepamba Moto Mfuko wa Pensheni Wa PSPF Kwakushirikiana na Ustawi wa Jamii wa Bagamoyo Wame Kabidhi Msaada wa Vitu mbalimbali Katika Kituo Cha Kulelea Watoto Yatima Cha AMANI kilichopo katika Mkoa Wa Pwani Wilaya Ya Bagamoyo Eneo la Zinga Baadhi Ya Zawadi na Msaada Ulio Tolewa ni pamoja na Mbuzi,Mchele,Unga wa sembe,Vinywaji na Mafuta ya Kula.
 
PSPF wameweza Kushiriki katika kutoa msaada Huo Ilikuweza kujenga mazingira mazuri kwa Watoto hao wanao lelewa katika vituo Mbalimbali na Kuwaweka karibu na Jamii Ili wasiweze kujihisi Katika hari ya Upweke Bali kuwa  Katika Hari Ya Furaha Hususani Katika Kipindi Hiki Cha Kusherehekea sikukuu ya Krismasi na Kuukaribisha Mwaka 
Akizungumza Wakati Wa Ugawaji Wa Zawadi na Msaada Huo Meneja wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF Mkoa wa Pwani Msafiri Mugaka amesema Mfuko wa PSPF ni mfuko Wa Jamii Unao Ungana na Jamii Mbalimbali Bila Kubagua Matabaka Yoyote Kwani Wao Wapo Kwaajiri ya Kusaidia Jamii Hivyo Kwa Kipindi Hiki wameamua Waanze na Kituo Cha Bagamoyo lakini Sio hapo tu Bali Wataendelea na Moyo Huo Ili kuhakikisha Watoto wanapata Mahitaji Machache Japo Havita watosha ila Vitawasaidia kwa kiasi kikubwa,Vilevile Aliwaasa watoto Wa Kituo Hicho Kwa Kuwaambia Siku Zote waendelee Kumtegemea Mwenyezi Mungu Kwani Ndiye anaye wawezesha kwa Yote atawakuza na Kuweza kufanya Kazi katika Mfuko Wa Pensheni Wa PSPF
Naye afisa Mahusiano wa Mfuko Wa Pensheni wa PSPF Coleta Mnyamani Alikuwa na Machache Ya Kuzungumza Wakati Wa Shughuli Ya Ugawaji Wa Zawadi na Msaada Ikiendelea "Kwaniaba Ya Makao Makuu ya PSPF Tunapenda Kushiriki Kuwasaidia Watoto Mbalimbali Wanaoishi Katika Mazingira Magumu Hata Wale wasio na Wazazi Hivyo Tunatoa Zawadi na msaada Huu Ili Kuweza Kuwakuza Watoto Ki Fikra na Kuto Dhani Kuwa Wao ni wapweke" Alimaliza Kwa Kusema Tunawapenda Watotop
 Wote Na Nijukumu La kila mmoja Kuwalea Ili Waweze Kuja Kuwa tegemezi kwa Baadae  
Mkurugenzi wa Kituo cha Kulelea watoto yatima Cha Amani Orphanage Centre  Magreth Mwegalawa Ametoa Shurani zake Za Dhati Kwa Niaba Ya Kituo Kwa Mfuko Wa PSPF Nimfuko nUnao Jali Jamii Kwani Ni Watu na Mashirika Machache Yenye moyo Kama Huu Tunapenda Kusema Asanteni na Muendelee Na Moyo Huo Huo Kwani Hawa Watoto ni Jukum letu kuwatimizia Ndoto Zao Mungu Awabariki Katika kazi zote muendeleazo kuzifanya .

No comments:

Post a Comment