Mazingira Yetu :Security Group (T ) Ltd (SGA) Wafanya Usafi Kuadhimisha Miaka 30 ya Utendaji kazi Nchini - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Monday, 15 December 2014

Mazingira Yetu :Security Group (T ) Ltd (SGA) Wafanya Usafi Kuadhimisha Miaka 30 ya Utendaji kazi Nchini

Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya ulinzi ya Security Group (T) Ltd (SGA), Eric Sambu akizungumza na wafanyakazi wa kampuni hiyo muda mfupi kabla ya kuanza kuufanyia usafi ufukwe wa Bahari ya Hindi, eneo la Mbezi Beach, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki kuadhimisha miaka 30 ya utendaji kazi wa kampuni hiyo nchini.
Wafanyakazi wa kampuni ya ulinzi ya ulinzi ya Security Group (T) Ltd (SGA), wakifanya usafi katika ufukwe wa Bahari ya Hindi, Mbezi Beach, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki kudhimisha miaka 30 ya kampuni hiyo tangu kuanza kufanya kazi zake hapa nchini.
Meneja Mawasiliano wa kampuni ya ulinzi ya Securty Group (T) Ltd (SGA), Sofia (kushoto) akitoa maelekezo kwa wafanyakazi wa kampuni hiyo wakati wa zoezi la kufanya usafi katika ufukwe wa Bahari ya Hindi, eneo la Mbezi Beach, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki ikiwa ni kuadhimisha miaka 30 ya utendaji kazi wa kampuni hiyo hapa nchini.
Wafanyakazi wa kampuni ya ulinzi ya Security Group (T) Ltd (SGA) akifurahia katika picha ya pamoja baada ya kukamilisha zoezi la ufanyaji usafi katika ufukwe wa Bahari ya Hindi, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki kuadhimisha miaka 30 ya utendaji kazi wa kampuni hiyo nchini.
Wafanyakazi wa kampuni ya ulinzi ya Security Group (T) Ltd (SGA) wakionesha sehemu ya taka ngumu walizookota katika ufukwe wa Bahari ya Hindi, eneo la Mbezi Beach, Dar es Salaam wakati walipoufanyia usafi ufukwe huo kuadhimisha miaka 30 ya utendaji kazi wa kampuni hiyo hapa nchini.

No comments:

Post a Comment