Habari na Jamii : PPF Yakutana na Wahariri wa Vyombo vya Habari , Mjini Bagamoyo - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Monday, 15 December 2014

Habari na Jamii : PPF Yakutana na Wahariri wa Vyombo vya Habari , Mjini Bagamoyo

Mkurugenzi wa Operesheni wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Asumpta Mallya, akionyesha tuzo ambayo PPF ilipata kwenye shindano la Afrika linaloandaliwa na taasisi ya ISSA, kuhusu utoajin bora wa huduma wa mifuko ya hifadhi ya jamii barani Afrika, hususan kwenye fao la elimu. Alikuwa akiwaonyesha wahariri wa vyombo vya habari kwenye semina ya siku moja iliyoandaliwa na Mfuko huo mjini Bagamoyo, mkoa wa Pwani Jumamlosi Desemba 13, 2014 baada ya kuibuka mshindi wa kwanza kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii kwa utoaji huduma bora kwa wanachama wake.Alikuwa akiwaonyesha wahariri wa vyombo vya habari kwenye semina ya siku moja ya Wahariri wa vyombo vya habari iliyofanyika mjini Bagamoyo , mkoa wa Pwani, Jumamosi Desemba 13, 2014.
Mkurugenzi wa Mifumo ya Computer wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Robert Mtendamema, akitoa mada kuhusu huduma za Mfuko huo zinavyotolewa kimtandao.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio, akitoa hotuba ya ufunguzi wa semina ya siku moja ya wahariri wa vyombo vya habari nchini, iliyofanyika Jumamosi Desemba 13, 2014, huko Bagamoyo mmkoani Pwani.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio, akizungumza kwenye semina ya simu moja ya wahariri wa vyombo vya habari iliyuolenga kutoa elimu zaidi ya huduma zitolewazo na Mfuko huo na mafanikio ambayo Mfuko imepata katika kipindi cha uhai wake. Semina hiyo ilifanyika mjini Bagamoyo, Jumamosi Desemba 13, 2014
Mkurugenzi wa fedha wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Martin Mmari, akionyesha tuzo ya ushindi wa jumla (Overall winner) ya utunzaji mahesabu inayotolewa na Bodi ya Ukaguzi wa Mahesabu (NBAA), hivi karibuni. Alikuwa akiwaonyesha wahariri wa vyombo vya habari waliokuwa wakishiriki semina ya siku moja iliyoandaliwa na Mfuko huo mjini Bagamoyo mkoa wa Pwani Jumamosi Desemba 13, 2014.
Mkurugenzi wa Uwekezaji wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Steven Alfred, akitoa mada kwenye semina hiyo.
Sehemu ya Wahariri waliohudhuliwa semina ya siku moja iliyoandaliwa na Mfuko huo mjini Bagamoyo mkoa wa Pwani Jumamosi Desemba 13, 2014.

No comments:

Post a Comment