Matukio Kitaifa :Dkt. Shein Awaapisha Kaimu Jaji Mkuu na Naibu Katibu Mkuu Afya Zanzibar - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Monday, 8 December 2014

Matukio Kitaifa :Dkt. Shein Awaapisha Kaimu Jaji Mkuu na Naibu Katibu Mkuu Afya Zanzibar


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Mkusa Issack Sepetu kuwa Kaimu Jaji Mkuu wa Mahakama Kuu ya Zanzibar katika hafla iliyofanyika leo Ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Halima Maulid Salum kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya katika hafla iliyofanyika leo Ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja.
Kaimu Jaji Mkuu wa Mahkama Kuu Zanzibar Jaji Mkusa Issack Sepetu na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Halima Maulid Salum wakiwa tayari kula kiapo cha Utii kwa Serikali ya Mapinduzi pamoja na Utekelezaji wa kazi zao Mpya watakazo pangiwa baada ya kuapishwa rasmi na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.
Naibu Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo (kulia) Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Abdalla Mwinyi Khamis (katkati) na Mshauri wa Rais Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Mzee Abrahman Mwinyi Jumbe wakiwa katika hafla ya kuapishwa Kaimu Jaji Mkuu wa Mahkama Kuu Zanzibar Jaji Mkusa Issack Sepetu na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Halima Maulid Salum Ikulu Mjini Unguja leo.
Baadhi ya Viongozi waliohudhurika katika hafla ya kupishwa Kaimu Jaji Mkuu wa Mahkama Kuu Zanzibar Jaji Mkusa Issack Sepetu na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Halima Maulid Salum wakifuatilia kwa makini wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipowaapisha leo Ikulu Mjini Unguja.[Picha na Ikulu.]

No comments:

Post a Comment