Kikosi
kazi maalum kutoka Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo
wakiongea na Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe
Bw.Lucas Mweri walimpotembelea leo ofisini kwake kwa ajili ya kufuatilia
na kufanya tathmini ya mikopo iliyokwishatolewa katika Halmashauri ya
wilaya ya Korogwe.
Mkurugenzi
mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe,Bw.Lucas Mweri akielezea
changamoto mbalimbali wanazopata kutoka katika Mfuko wa maendeleo ya
Vijana ikiwemo fedhaza mkopo kuwa ndogo, kwa kikosi kazi kutoka Wizara
ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo walipomtembelea ofisini kwake leo
kufuatilia na kufanya tathmini ya mikopo iliyokwishatolewa kutoka Mfuko
wa Maendeleo ya Vijana.
Afisa
Uchumi Mwandamizi kutoka Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na
Michezo,Bw.Yohana Ngao akiongea na wajumbe wa kikundi cha HEKIMA
walipowatembea leo katika kata ya Mazinde kujua changamoto gani
wanakutana nazo tangu wapewe mikopo kutoka katika mfuko wa Maendeleo ya
Vijana.
Afisa
Maendeleo ya Jamii Bi.Sabitina Maneto akitoa maoni kwa Kikosi kazi
kutoka Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo(hawapo
Pichani),kuhusu jinsi ya kuboresha mfuko wa Maendeleo ya Vijana na
Kuufanya uwe bora zaidi uku akikazia pesa kwenda moja kwa moja kwenye
SACCOS baada ya kuja kwenye vikundi.
Wajumbe
wa kikundi cha HEKIMA kutoka kata ya Muheza wakiwa katika picha ya
pamoja na wajumbe wa kikosi kazi kutoka Wizara ya
Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo walipowatembea leo ili kufanya
ufuatiliaji na tathmini ya mikopo iliyokwishatolewa kwa kikundi hicho.
Mjumbe
wa kikundi cha HEKIMA kata ya Mazinde Rashid Salum(mwenye shati la
bluu),akiwaonyesha Mradi wa Matofali uliotokana na pesa za Mfuko wa
Maendeleo ya Vijana,Bw.Yohana Ngao ambae ni Afisa Uchumi Mwandamizi
kutoka Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo(katikati) na Afisa
Maendeleo ya Vijana Halmashauri ya Wizara ya Korogwe Bw.Mhinzi.
Wajumbe
wa Kikosi kazi kutoka Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo
wakiskiliza kwa makini maelezo kutoka kwa Katibu wa kikundi kisicho cha
kiserikali-MOIDES(hayupo pichani),Bw.Nurdin Imam jinsi walivyotumia pesa
walizopewa kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Vijana.
Afisa
Uchumi Mwandamizi kutoka Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na
Michezo,Bw.Yohana Ngao(wa kwanza kulia) akiskiliza maoni kutoka kikundi
cha Nyota Alfajiri ambao wameanzisha mradi wa kutengeneza Matofali na
kuuza Asali ambapo walichukua mkopo wa shilingi milioni mbili na
kurudisha kiasi cha shilingi laki 732,000 wakiwa wamefata taratibu zote
za kurudisha mkopo ndani ya mwezi mmoja.
Wajumbe
wa Kikosi kazi kutoka Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo
wakiaangalia moja ya mradi wa matofali kutoka kikundi cha Nyota Alfajiri
uliofanikiwa kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana.Kikundi hicho
kimetengeneza matofali elfu kumi na nne(14,000) na wanajiandaa kuyauza
ili kujiendeleza kimaisha.
No comments:
Post a Comment