Waziri
wa Maliasili na Utalii, Mhe. Lazaro Nyalandu, amesema habari zinazodai
kuwa Serikali inataka kuwaondoa wakazi wa zaidi ya 40,000 katika eneo la
Loliondo, Ngorongoro mkoani Arusha hazina ukweli wowote.
Novemba
mwaka huu, gazeti The Guardian la nchini Uingereza, liliandika habari
kuwa serikali ina mpango wa kuwafukuza Wamasai wanaoishi eneo hilo.
Gazeti hilo lilidai kuwa, lengo ni kuwapatia eneo lenye kilometa za mraba 1,500, kampuni ya OBC ya Falme za Kiarabu.
Akizungumza
na wananchi wa jamii ya kimasai wilayani Ngorongoro mwishoni mwa wiki,
Nyalandu alisema habari hizo hazina ukweli wowote isipokuwa zina lengo
la kuchafua taswira nzuri ya nchi yetu kimataifa.
Aliwataka wakazi wa eneo hilo kuishi bila hofu, kwa sababu serikali haina mpango wa kuwaondoa kwenye makazi yao.
“Nami
niwahakikishie wanajamii wa Loliondo, Ngorongoro na wanajamii wote wa
kimasai ambao wametishiwa nyau, kuwa serikali ya Tanzania haina mpango
wowote wa kumfuata na kumfukuza mtu yoyote,” alisema.
Waziri
wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu akijaribu kurusha mkuki
alipotembelea eneo la Loliondo wilayani Ngorongoro kukanusha uvumi juu
ya kuondolewa kwa Jamii ya Wamasai katika eneo hilo.
Waziri
wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu akitoka nje ya nyumba ya
kimasai alipotembelea eneo la Loliondo wilayani Ngorongoro kukanusha
uvumi juu ya kuondolewa kwa Jamii ya Wamasai katika eneo hilo.
Waziri
wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu akionja maji kutoka katika
kisima kilichojengwa kwa ajili ya kutatua tatizo la maji katika katika
eneo la Loliondo.
Waziri
wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu akiongea na Wamasai
waliokusanyika kwa ajili ya kusikia tamko la serikali juu ya uvumi wa
kuondolewa kwa Jamii ya Wamasai katika eneo hilo.
Wamasai wakichukua kumbukumbu muhimu katika mkutano wao na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu.
Waziri
wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu akiwa katika picha ya
pamoja na baadhi ya wanawake wa jamii ya kimasai mara baada ya kumaliza
mkutano nao.
Makamu
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro Raphael Rong’oi
akizungumza na wananchi wa jamii ya kimasai kabla ya kumkaribisha Waziri
wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu (aliyekaa kwenye pikipiki).
Waziri
wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu akiagana na mzee wa kimasai
mara baada ya kumaliza mkutano uliokuwa na lengo la kukanusha uvumi juu
ya kuondolewa kwa jamii ya Wamasai katika eneo hilo.
No comments:
Post a Comment