Wakaguzi
wa Miradi ya Maendeleo toka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wamepata
fursa adhimu ya kutembelea meli kongwe kupita zote nchini, MV Liemba
iliyo kwenye Ziwa Tanganyika, mkoani Kigoma.
Wakizungumza
mara walipofika katika meli hiyo baadhi ya wakaguzi hao hawakuficha
bashasha waliyokuwa nayo mara baada ya kuingia ndani ya meli hiyo kongwe
iliyo na umri zaidi ya miaka 100.
Mmoja
wa wakaguzi hao Bibi Zena Hussein, alisema kuwa anajisikia furaha sana
kuingia na kushuhudia mandhari ya meli hiyo ya kihistoria nchini
Tanzania.
“Nimefurahi
sana kufika leo hii kwenye meli hii yenye miaka zaidi ya 100, licha ya
ukongwe wake bado inaonekana imara na yenye uwezo wa kufanya kazi miaka
mingi zaidi,” alisema.
MV
Liemba ni meli ya Kitanzania inayohudumia pwani za Ziwa Tanganyika. Ni
chombo cha usafiri wa majini chenye umri mkubwa kuliko kingine chochote
nchini na kipo tangu mwaka 1914. Meli hii kama zilivyo meli ningine
inasukumwa na injini ya diseli na ina urefu wake ni mita 67, upana mita
10 na uzito wa tani 1500.
Kwa mujibu wa Nahodha wa meli hiyo, Kapteni Mathew Mwanjisi, meli hiyo ina uwezzo wa kubeba abiria 600 na tani za mizigo 200.
“Katika daraja la kwanza meli ina uwezo wa kubeba abiria 20, daraja la pili abiria 30 na daraja la tatu abiria 550,” alisema.
Meli
ya MV. Liemba inamilikiwa na Kampuni ya MSCL na kusajiliwa na Mamlaka ya
Usafiri Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) kwa namba ya usajili KP/P001.
Meli hiyo ilijengwa katika Bandari ya Kigoma mwaka 1913 na mjenzi kutoka
Ujerumani kwa ajili ya usafirishaji wa mizigo na abiria.
Mv.
Liemba ilitengenezwa nchini Ujerumani mwaka 1913 ikiwa ikiitwa kwa
Kijerumani "Graf von Goetzen" kwenye kiwanda cha meli cha Meyer huko
Papenburg.
Timu
ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango
ikiwa ndani ya MV Liemba mara walipofika kujionea mandhari ya meli hiyo
kongwe duniani.
Kiongozi
wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya
Mipango, Bibi Florence Mwanri (Kushoto) akisaini kitabu cha wageni
ndani ya MV Liemba. Kulia ni Nahodha wa Meli hiyo, Kapteni Mathew
Mwanjisi.
Nahodha
wa MV Liemba, Kapteni Mathew Mwanjisi (Watatu kushoto) akitoa maelezo
kwa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya
Mipango.
Kiongozi
wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya
Mipango, Bibi Florence Mwanri (Wapili Kulia) akiiongoza Timu yake
kusikiliza kwa umakini namna ya kusoma radar inayotumika ndani ya Meli
ya MV Liemba. Anayewapa maelezo ni Nahodha wa Meli hiyo, Kapteni Mathew
Mwanjisi.
Nahodha
wa Meli ya MV Liemba, Kapteni Mathew Mwanjisi (Kulia) akitoa maelezo ya
namna ya kutumia chombo cha kuokolea kwa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya
Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango. Wanaomsikiliza ni
Kiongozi wa Timu hiyo, Bibi Florence Mwanri (Kushoto) na Kaimu
Mkurugenzi wa Mipango na Ufuatiliaji (Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango),
Bw. Omary Abdallah.
Mhandisi
Mkuu wa Meli ya MV Liemba, Eng. Justine Joachim (Mwenye fulana nyeusi)
akiwapa maelezo Wakaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais,
Tume ya Mipango walipongia kujionea mitambo ya kuendeshea meli hiyo.
Kazi inaendelea! Watumishi wa Meli ya MV Liemba wakiendelea na kazi ya kushusha shehena ya mahindi kutoka kwenye meli hiyo.
PICHA NA SAIDI MKABAKULI
No comments:
Post a Comment