Wanamichezo wakimsikiliza kwa makini Waziri Membe (Hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao. Viongozi mbalimbali wa vyama vya michezo wakimsikiliza Waziri Membe (hayupo pichani). |
Wakwanza Kushoto ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Mambo ya Nje, Bw.Mkumbwa Ally, na wapili kutoka kushoto ni Afisa Mambo ya Nje Bw. Imani Njalikai wakifuatilia kikao kati ya Waziri Membe na wanamichezo walio shiriki michezo ya jumuiya ya madola Glasgow, Scotland. |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe (Mb.) akisaini kwenye kitabu cha wageni alipo wasili katika kituo cha Filbert Bayi kilichopo Kibaha Mkuza. |
Katikati ni Mama Bayi akielezea jambo kwa waziri Membe (wa kwanza kulia) mara baada ya kusaini kitabu cha wageni, wakwanza kulia ni Bw. Filbert Bayi naye akisikiliza. |
Bw. Filbert Bayi akimwonyesha na kumwelezea Waziri Membe Ramani ya eneo lililo na Shule ya awali, msingi, Sekondari na kituo cha michezo cha Filbert Bayi, lililopo Kibaha Mkuza. |
Waziri Membe akizungumza alipokuwa akitazama kiwanja cha mpira wa miguu (hakipo pichani), kiwanja hicho cha mpira ni moja kati ya viwanja vinavyotumiwa na wanamichezo waliopo katika kituo hicho cha Filbert Bayi. |
Kiwanja cha mpira wa miguu kilichopo katika kituo cha michezo cha Filbert Bayi. |
Waziri
Membe akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa vyama vya michezo
mbalimbali nchini, mara baada ya kumaliza kikao na wanamichezo.Picha na Reginald Philip
=========================================
Mhe. Membe Aahidi Kuendeleza Diplomasia ya Michezo
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe,
amewataka wanamichezo wa Tanzania kutokata tama kwa kufanya vibaya
kwenye michezo ya Jumuiya ya Madola mwaka huu, na kuahidi kuendelea
kupigania maendeleo ya sekta hiyo.
Akiongea
katika kiko cha kutathmini matokeo ya timu ya Tanzania, ambayo
haikushinda medali yoyote kwenye michezo hiyo ya Madola, iliyomalizika
mjini Glasgow, Scotland mwezi Agosti, Mhe. Membe alisema wizara yake
itafanya juhudi zaidi kutafuta wadhamini wa matayarisho ya timu ya taifa
ndani na nje ya nchi, chini ya mkakati wa diplomasia ya michezo.
Kikao
hicho kilichohudhuriwa na viongozi wa vyama vya michezo na baadhi ya
wanamichezo walioshiriki michezo ya Glasgow, kilifanyika leo kwenye
kituo cha michezo cha Filbert Bayi Mkuza.
''Msikatishwe
tamaa na matokeo mabaya ya Glasgow, kwani mara nyingi mafanikio huja
mara ya pili,'' alisema Mhe. Membe, na kuongeza: ''Tutumie yale
yuliyojifunza kwa kushindwa hukokupanga wakati wa ushindi katika
mashindano yajayo.''
Mhe.
Waziri aliisifu timu ya Tanzania kwa kuonyesha nidhamu ya hali ya juu
iliposhiriki michezo ya Madola, lakini akasisitiza kuwa nidhamu peke
yake haitoshi. ''Nidhamu hiyo ituletee ushindi.'' alisema.
Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, kwakushirikiana na Wizara
ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, ilitafuta udhamini wa kambi za
mazoezi kwa miezi miwili kwa wanamichezo wa timu ya taifa huko Uturuki,
China, Ethiopia, na New Zeland, kabla ya kwenda Glasgow.
Katibu
Mkuu wa kamati ya Olimpiki ya Tanzania, Bw. Filbert Bayi, alisema
kufanya vibaya kwa timu hiyo kulichangiwa na muda mfupi wa kukaa kambini
na kukosa mashindano ya kujipima nguvu. Ali9shauri idadi ya washiriki
na michezo vipunguzwe kulingana na uwezo wa taifa kifedha.
Mkurugenzi
wa Michezo, ambaye aliongoza msafara wa Glasgow, Bw. Leornard Thadeo,
alisema timu ya Tanzania ilikuwa na ushindani hafifu kutokana na mafunzo
hafifu, viwango vya chini vya wachezaji, ukosefu wa vifaa na kuchelewa
kutolewa fedha za uwezeshaji.
Walimu
wa michezo na wachezaji walisisitiza matayarisho ya muda mrefu zaidi,
mazingira mazuri ya mazoezi na udhamini mpana zaidi utakaohusisha
taasisi za umma na binafsi.
|
No comments:
Post a Comment