Meneja Kanda ya Kaskazini wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, Rajabu Kinande, akizungumza
na Waandishi wa habari mjini Arusha, kuhusu Mkutano wa 7 wa Wadau wa
LAPF, unaokwenda sambamba na maadhimisho ya miaka 70 tangu kuanzishwa
kwa Mfuko huo wa Pensheni wa LAPF. Kushoto ni Meneja LAPF Kanda ya Dar
es Salaam, Amina Kassim, na Meneja Masoko wa LAPF, James Mlowe.
Meneja
Kanda ya Dar es Salaam wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, Amina
Kassim akizungumza na Waandishi wa habari mjini Arusha, kuhusu Mkutano
wa 7 wa Wadau wa LAPF, unaokwenda sambamba na maadhimisho ya miaka 70
tangu kuanzishwa kwa Mfuko huo wa Pensheni wa LAPF. Kushoto ni Meneja
Masoko wa LAPF, James Mlowe na Kulia ni Meneja wa LAPF Kanda ya
Kaskazini. Rajabu Kinande.
****************************************************
Maandalizi
ya Mkutano Mkuu wa Saba wa wadau wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF,
yamekamilika ambapo mkutano huo utahudhuriwa na wajumbe zaidi ya 700
toka nchini na nje ya nchi.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo mjini Arusha, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa
Pensheni wa LAPF Bw. Eliud Sanga, amesema maadalizi yote ya mkutano huo,
wenye kauli mbiu ya "Maadhimisho ya Miaka 70 ya Ukuaji na Huduma Bora,
LAPF", yamekamilika ambapo ambapo utakwenda sambamba na maadhimisho ya
miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Mfuko huo wa Pensheni wa LAPF.
Bwana
Sanga amesema Mfuko wa LAPF ndio mfuko unaoongozwa sii tuu kwa kutoa
mafao bora, bali pia ndio mfuko unaoongoza kwa kuwa na afya bora kabisa
ambapo kwa sasa una rasilimali zenye thamani ya shilingi bilioni 700,
LAPF ndio mfuko unaoongoza kukua kwa kasi zaidi ambapo unakuwa kwa
asilimia 21 kwa mwaka!.
Ameendelea
kutoa sifa za LAPF kuwa ni pamoja na kuwa ndio mfuko unaolipa kwa
haraka zaidi, ambapo mstafuu kama anastaafu kesho, LAPF wao wanalipa
jana!.
Bwana
Sanga hakuishia hapo, amesema LAPF ndio mfuko unaoongoza kwa utunzani
wa mahesabu kati ya mifuko yote kwa mujibu wa NBAA, na ndio mfuko
unaokuwa kwa kasi zaidi kwa mujibu wa SSRA!.
Mkutano
huo, utafunguliwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Hawa Ghasia, na Kufungwa na Waziri wa
Kazi na Ajira, Mhe. Gaudensia Kabaka.
No comments:
Post a Comment