Serikali
imeamua kuanzisha usajili mpya wa namba za pikipiki (aina zote za
pikipiki zenye magurudumu mawili na zile za magurudumu matatu) ili
kurahisisha usimamizi na utawala wa vyombo vya moto.Utaratibu mpya
unaanza rasmi tarehe 1/10/2014, Mmiliki anapewa muda wa miezi sita
kusajili chombo cha moto bila adhabu.
Utaratibu
huu utahusu chombo cha moto chenye magurudumu mawili hadi matatu.
Chombo cha moto kitakachotumika kwa ajili ya biashara kitapewa kibao cha
rangi nyeupe na chombo kwa ajili ya shughuli binafsi kitapewa kibao cha
namba ya njano.
Usajili
huu utafanyika katika ofisi zote za TRA naMmiliki anatakiwa kwenda
TRA na kadi halisi ya gari na Tshs.10, 000/- kwa ajili ya kadi mpya.
No comments:
Post a Comment