Mwenyekiti
wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), Dk. Martern Lumbanga
(kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es
Salaam jana, kuhusu matokeo ya ukaguzi wa shughuli za ununuzi katika
taasisi za umma uliofanywa na PPRA kwa mwaka wa fedha ulioishia Juni 30
mwaka huu. Kulia ni Mjumbe wa Bodi ya PPRA, Jaji mstaafu, Thomas Mihayo.
Mjumbe wa Bodi ya PPRA, Jaji mstaafu, Thomas Mihayo akizungumza katika mkutano huo.
Wajumbe
wa Bodi wakiwa kwenye mkutano huo. Kutoka kushoto ni Mhandisi Leonard
Chamuriho, Profesa Silvia Temu na Mhandisi Boniface Muhegi.
Maofisa mbalimbali wa Sekretarieti ya PPRA wakiwa kwenye mkutano huo.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Na Dotto Mwaibale
MAMLAKA ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), imesema taasisi 13 ilizozikagua manunuzi yake yalikuwa na viashiria vya rushwa.
Hayo
yalibainishwa na Mwenyekiti wa Bodi ya PPRA, Dk. Martern Lumbanga wakati
akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, kuhusu matokeo
ya ukaguzi wa shughuli za ununuzi katika taasisi za umma uliofanywa na
PPRA kwa mwaka wa fedha ulioishia Juni 30 mwaka huu.
"Taasisi hizo zilionekana kuwa na viwango vya zaidi ya asilimia 20 ya viashiria vya rushwa" alisema Lumbaga.
Lumbanga
alizitaja taasisi hizo kuwa ni Halmshauri ya Wilaya ya Kondoa, Kilwa,
Kishapu, Monduli, Maswa, Mamlaka ya Maji na Mazingira Lindi, Wizara ya
Afya na Ustawi wa Jamii na Ofisi ya Katibu Tawala ya Mkoa wa Lindi.
Alitaja
taasisi zingine kuwa ni Halmshauri ya jiji la Mwanza, Halmshauri ya
jiji la Dar es Salaam, Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere,
Halmshauri ya Manispaa ya Musoma na Halmshauri ya Manispaa ya Kinondoni.
Alisema
hatua iliyofikiwa na PPRA kwa taasisi hizo ni kutoa taarifa kwa Taasisi
ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (PCCB) ili kufanya uchunguzi zaidi na
kuchukua hatua kwa taasisi hizo.
Katika
hatua nyingine PPRA imezifungia kampuni 19 kushiriki zabuni kwenye
taasisi za umma nchini kutokana na kushindwa kutekeleza kikamilifu
mikataba zilizoingia na taasisi za umma na hivyo kusababisha mikataba
hiyo kuvunjwa.
Alisema
Bodi ya PPRA imezisimamisha kampuni nne kushiriki katika zabuni za umma
kwa muda mpaka pale mchakato wa kuzifungia au la utakapofikiwa.
Lumbanga
alizitaja taasisi zilizofanya vibaya katika manunuzi ya umma kuwa ni
Mamlaka ya Maji na Mazingira Lindi (Uwasa), Halmsahauri ya Wilaya ya
Kishapu, Kibondo, Kilindi, Lushoto na Ofisi ya Katibu Tawala ya Mkoa wa
Lindi.
No comments:
Post a Comment