Afisa
Ushauri wa Vijana wa UNFPA – Tanzania Bi. Farida Juma malezo kuhusu njia
sahihi ya matumizi ya Kondomu kwa baadhi ya vijana waliotembelea banda
la UNFPA katika viwanja vya Maonyesh ya Wiki ya Vijana yanayofanyika
mjini Tabora.
Mkuu
wa Kitengo cha Sheria wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
Bibi. Esther Riwa akigawa jarida la Si Mchezo kwa mmoja wa wananchi
aliyetembelea banda la Wizara hiyo katika Maonyesho ya Wiki ya Vijana
mjini Tabora.
Afisa
Utamaduni wa Bodi ya Filamu Tanzania Bw. Simon Peter akielezea kuhusu
namna ya uandishi wa miswada ya Filamu kwa mmoja wa vijana
awaliotembelea banda lao katika Maonyesho ya Wiki ya Vijana mjini
Tabora.
Afisa
Vijana Mstaafu akitoa mada kuhusu Stadi za Maisha katika Kongamano la
Vijana ikiwa ni kuadhimisha Wiki ya Vijana ambao Kitaifa inafanyikia
mkoani Tabora.
Baadhi
ya wadau wa Vijana wakifuatilia mada wakati wa Kongamano la Vijana
kuhusu Stadi za Maisha lililofanyika mjini Tabora mapema hivi karibuni.
Vijana wa DSW wakifafanua kuhusu progamu ya Kijana Kwa Kijana inayoendeshwa na Shirika lao kwa kushirikisha vikundi vya vijana.
Baadhi
ya Watumishi waWizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
wakiangalia Vitabu wakati wa Maonyesho ya Wiki ya Vijana mjini Tabora.
Wadau wakiangalia Kahawa ya Ngara katika banda la Mkoa wa Kagera.
Mjasiriamali
wa Mikoba na Batiki Bibi. Sophia Labani akimwelekeza mteja wake ubora
wa bidhaa zake wakati wa Wiki ya Vijana inayofanyika kitaifa mjini
Tabora.
Picha Na Frank Shija, Tabora.
No comments:
Post a Comment